Goli la Simba limefungwa na Amis Kiiza katika dakika ya nane kipindi cha kwanza bao ambalo limedumu hadi dakika ya 90 ya mchezo na kuishuhudia Simba ikiondoka uwanjani na pointi tatu mbele ya Mtibwa.
Kikosi cha Simba kilikuwa chini ya kocha Jackson Mayanja aliyejiunga hivi karibuni kama kocha msaidizi wa timu hiyo kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa kocha msaidizi wa wekundu wa Msimbazi Selemani Matola ambaye alijiuzulu kutokana na kutoelewa na aliyekuwa kocha mkuu Dylan Kerr.
Baada ya kuondoka kwa Kerr Mayanja alipewa jukumu la kuinoa Simba akiwa kama kocha mkuu hadi hapo atakapopatikana kocha mkuu atakayechukua mikoba ya Kerr aliyetimuliwa baada kufungwa na Mtibwa Sugar kwenye michuano ya Mapinduzi Cup wiki iliyopita visiwani Zanzibar.
Mchezo huo ulikuwa ni kwanza kwa Mayanja na amefanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya timu iliyowatoa kwenye Mapinduzi Cup wakati huo Mayanja alikuwa jukwaani akishuhudia mtanange huo. Ushindi wa leo wa kikosi cha Simba ni sawa na kulipa kisasi kwa wakatamiwa hao.
Mtibwa Sugar walicheza soka safi licha ya kupoteza mchezo huo lakinin watajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi walizozipata kwenye mchezo huo.
Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa leo kwenye viwanja vingine ni kama ifuatavyo:
JKT Ruvu 1 – 5 Mgambo JKT
Toto Africans 0-1 Tanzania Prisons
Stand United 1-0 Kagera Sugar
Mbeya City 1-0 Mwadui FC
Coastal Union 1-1 Maji Maji FC
No comments:
Post a Comment
paulmkale