Abdu Kiba adai wasanii wa WCB wanabebwa na Promo
Abdu Kiba amesema kuwa promotion ndiyo inawabeba wasanii wa lebo ya WCB.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha XXL
cha Clouds FM, “Sijafikiria kuimba na msanii kutoka WCB, kwa sababu
sijaona anayeimba type ya muziki wangu.”
“Hata kama wana promote kwa sababu ndiyo
walipoona wao ndiyo wanaweza wakafanya na watu wakaweza kuelewa lakini
siku zote ajuae hazami,” alisema Abdu Kiba.
Aidha aliongeza kuwa bado hajaona msanii anayeimba type ya muziki wake ndani ya lebo hiyo [WCB].
Hata hivyo mapema mwezi huu msanii huyo
alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa yupo tayari
kujiunga na lebo wa WCB kama watakubaliana na kuweka hela mezani kauli
ambayo baadaye yeye mwenyewe aliipinga kuwa watu hawakumuelewa vizuri
alichomaanisha.
No comments:
Post a Comment
paulmkale