Barakah Da Prince ajiunga na Rockstar4000 ambayo Yupo Alikiba na Lady Jaydee
Hitmaker wa Siwezi, Barakah Da Prince amesainishwa mkataba wa usimamizi na kampuni ya Rockastar4000.
Ameungana
na Alikiba na Lady Jaydee kuwa msanii wa tatu kuwa chini ya uongozi
huo. Na kwa sasa muimbaji huyo atakuwa akijulikana kama ‘Barakah The
Prince.’
Kwenye maelezo yake, CEO na mwanzilishi wa label hiyo,
Jandre Louw amedai kufurahishwa kumsaini muimbaji huyo wa Mwanza na
kumwelezea kama mwenye kipaji cha hali ya juu.
Akiwa
chini ya label hiyo, Barakah ataanza kuandaa album yake ya kwanza
itakayotoka mwaka 2017.Muimbaji huyo amejipatia umaarufu kwa nyimbo zake
kama Siachani Nawe, Nivumilie na Siwezi.
No comments:
Post a Comment
paulmkale