KARIA AWAPA YANGA SAA 48 TU KUTENGUA MAAMUZI YA KUJIONDOA KAGAME CUP




Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia amewataka Yanga kutengua ombi lao ndani ya saa 48 la kutaka wasishiriki michuano ya Kombe la KAGAME inayotarajia kuanza Juni 28 2018 jijini Dar es Salaam.

Hatua ya imekuja kufuatia uongozi wa klabu hiyo kutuma barua inayoeleza kuomba kujitoa ili kuwapa wachezaji wake mapumziko kwa ajili ya kuja kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC.

Karia amefunguka kwa kuwapa Yanga saa 48 kwa maana ya siku mbili kuanzia leo kutengua kauli hiyo akieleza kuwa hata Gor Mahia ambao wapo kundi moja CAF pamoja na Rayon Sports wamethibitisha kushiriki.

Rais huyo ameongea kauli hiyo kwa msisitizo akiamini Yanga wanaweza kubadilisha maamuzi hayo aliyosema hayana mashiko ili kuungana na wenzao Simba ambao wamepangwa kundi moja kushiriki mashindano hayo yatakayomalizika Julai 13.

Yanga walituma barua hiyo TFF juzi wakiomba kujiondoa kwenye mashindano hayo kwa lengo la kuwapa wachezaji nafasi kujiandaa katika michuano ya CAF ambapo Julai 18 Julai 2018 watacheza na Gor Mahia huko Kenya.

No comments:

Post a Comment

paulmkale