Akizungumza na Bongo5 jana akiwa jijini Mwanza kwaajili ya Serengeti Fiesta 2014, Dogo Janja amedai kuwa tayari ameshaanza mafunzo ya kutumia vyombo vya muziki kama vinanda.
“Mimi napenda sana muziki, shule yenyewe basi nitaangalia mbeleni huko,” amesema rapper huyo. “Mimi hakuna maishani kwangu ninachokipenda kama muziki,nataka kwenda kusomea muziki, nishaanza kupiga vinanda, kuna chuo cha muziki na kuna mwalimu ananifunza anaitwa David. Kwahiyo nitaongeza juhudi zaidi kwenye kujifunza muziki kwa sababu ni kitu ambacho nakiweza na ninakipenda. Wadau wangu na wapenzi wa burudani wasubiri ujio wangu mpya ambao utakuwa na muziki mzuri,” ameongeza.
No comments:
Post a Comment
paulmkale