Add caption |
Katika nchi za Guinea na Liberia, baadhi ya maiti zimekuwa zikionekana kutelekezwa mitaani huku wagonjwa wengine nao wakianguka na wasipe msaada.Wanajeshi wa Liberia wameweka kizuizi kuwazuia watu kutoka mikoa ya magharibi iliyoathirika na ugonjwa huo wasiingie kwenye mji mkuu Monrovia. Mwaka huu pekee ugonjwa huo umeua watu 930 Afrika Magharibi.Nchini Sierra Leone wanajeshi nao wameweka vizuizi kuzuia watu kutoka maeneo ya mashariki yaliyoathirika.Huo ni mlipuko mkubwa zaidi wa ugonjwa huo kuwahi kutokea na shirika la afya duniani lifanya mkutano wa siku mbili kuamua kutangaza kuwa ni dharura ya kiafya ya dunia.
No comments:
Post a Comment
paulmkale