Msanii
wa bongo fleva, Ommy Dimpoz, amefunguka kuhusiana na picha zilizozua
utata na kuzozagaa mitandao zikimuonesha akiwa kitandani na msanii wa
filamu Wema sepetu.
Ommy amesema kuwa hana maelezo zaidi ya kuzungumza zaidi ya kusema kuwa hajui ni muda upi zilipigwa picha hizo.
Wiki hii picha hizo zilisambaa mitandaoni na kuzua maswali kuwa Ommy
Dimpoz, ameamua kujiweka kwa Wema, baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi
wake Diamond Platinum."Ni
picha tu mimi naona kama ni picha zingine tu za kawaida, sasa
nimeshindwa kuelewa kwanini labda zimetengeneza sana stori kwasababu
mimi naona sio mara yangu kwanza kupiga picha na Wema hata uki google
utaona tunapicha nyingi sana kwa hiyo sijaelewa kwanini zimeleta stori
May
be nafikikiri zilizotengeneza stori zaidi ni hizi ambazo zinaonesha
tuko chumbani kwasababu mimi nilikuwa nimelala kiukweli na tulikuwa
tunakaa kwenye apartment moja nilikua nimeshtukia picha zipo kwenye
mitandao unajua unavyokaa kwenye apartment kwasababu tulienda kwenye
matembezi binafsi na washikaji wengine tulikua wengi wengi kidogo
tulienda South Africa unajua mnavyokaa kama familia kunakuwa na mambo ya
utani utani nimeshtukia tu picha zimeenea kwahiyo hata watu wakiniuliza
ninawambia wamuuliza aliyepiga picha hizo," Alisema Dimpoz.
Wengi wanafahamu kuwa wewe ni mshikaji wa Diamond Platnumz imekuaje
sasa hivi kuonekana kwenye picha na Ex wa Diamond Platnumz,Wema
Sepetu…?”
Ommy
Dimpoz ; “…Sidhani kama kuna tatizo kwasababu hawa wote ni watu wangu
nimefahamia nao siku nyingi nimekuwa nao karibu katika kipindi tofauti
kabla hawajakuwa kwenye uhusiano mimi tayari ni watu wangu sidhani mimi
nianze kuelezea sijui ooh nilikuwa labda na Wema sehemu, Wema ni
mshikaji wangu tangia siku nyingi kwa hiyo hata kama alikuwa katika
uhusiano na Diamond yakatokea mahusiano yao pengine hayapo sasa hivi
hayawezi kunifanya mimi kuharibu ushikaji wangu kwasababu hivyo ni vitu
vyao personal…"Alisema.
No comments:
Post a Comment
paulmkale