SIKU chache
baada ya Nasibu Abdul ‘Diamond’ kuweka picha zinazomuonesha mpenzi wake
wa sasa Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na kitumbo
kinachoashiria kukua kwa ujauzito, mama mzazi wa zilipendwa wa Diamond,
Wema Sepetu ‘Madam’, Mariam Sepetu amefunguka kuwa amefurahia tukio
hilo.
Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Mzazi huyo ambaye ni fundi wa kuzungumza, alisema tukio hilo
limemfurahisha kwani anaamini ndoto za Diamond kurudiana na binti yake
zitakuwa zimeyeyuka rasmi kama alivyokuwa akimuomba Mungu siku zote.
Kuonesha kwamba amefurahishwa na kitendo hicho, alimtaka Zari aendelee
kumpenda Diamond, amgande kila idara ili isije kutokea akarudi kwa binti
yake ambaye walimwagana mwishoni mwa mwaka jana.
“Yaani kama inawezekana naomba sana huyo Zari azidi kumganda Diamond,
asimpe muda wa kugeuka nyuma kabisa ili mambo mengine yaendelee kwa
sababu uhusiano wa Diamond na mwanangu haukuwa na baraka zangu,” alisema
mama Wema.
Mama
Sepetu aliongeza kuwa, hana maana ya kumchagulia mchumba mwanaye bali
anahitaji mwanaume yeyote mwenye heshima na anayejiheshimu kwa sababu
mwanaume asiyejitambua hawezi kuwa baba bora wa familia.

Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akiwa na mama yake, Mariam Sepetu.
“Sio kwamba namchagulia mtoto wangu mume gani amuoe lakini nahitaji mtu
mwenye heshima na kujiheshimu mwenyewe ndio anaweza kuwa baba wa familia
la sivyo inakuwa ni mambo ya kihunihuni tu kama ilivyokuwa kwa
Diamond.”
Alipotafutwa Diamond kuhusiana na kauli hiyo ya mama Wema, simu yake
iliita bila kupokelewa lakini kupitia ukurasa wake wa Instagram, staa
huyo wa Wimbo wa Mdogomdogo, alitupia picha ya Zari huku akizungushia
duara tumboni na kuandika; ‘kileee kinaanza kumharibia mtu mavazi.’
No comments:
Post a Comment
paulmkale