Timbulo kukimbiwa na Promota Mwanza Hekaheka FEB20

Ijumaa ya February 20, nimekurekodia Hekaheka ya leo inamhusu Timbulo ambaye amezungumzia kisa alichokutana nacho mwaka jana, ishu ni kukimbiwa na promota aliyemuita kwenye show.

Timbulo alikuwa kwenye show Kahama kulikuwa na promota ambaye aliandaa show na wasanii wengine na hawakuja, akaongea na Timbulo ili aende kwenye show hiyo kama njia ya kuziba pengo hilo.

Baada ya kufika wakaanza maandalizi ya mwisho mwisho ikiwemo kufanya matangazo ya barabarani kwenye gari, Timbulo akaomba alipwe chake kabla ya show jamaa akawa kama anakwepa, baadaye jamaa akakimbia kabisa, ili kujiweka upande salama Timbulo aliripoti Polisi ili wadili na ishu hiyo halafu yeye akaondoka zake.

No comments:

Post a Comment

paulmkale