(Picha: humanium.org)
MKUU wa
Mkoa wa Rukwa, Magalulla Said Magalulla amewataka wazazi na walezi
mkoani humo kuhakikisha watoto wao wenye sifa za kuanza masomo
wanakwenda shule mara tu zitakapofunguliwa hata kama hawana sare.
Magalulla
alisema kuwa hakuna visingizio tena vya watoto kushindwa kuhudhuria
masomo kwa madai wazazi hawana uwezo kwa sababu tayari Rais John
Magufuli ametangaza elimu bure kuanzia elimu ya awali hadi sekondari.
“Mahitaji
mengine mtoto atayapata akiwa tayari shuleni lakini sio mzazi au mlezi
asubiri mpaka amtimizie mahitaji yote. Wazazi kwanza wapelekeni watoto
wote waliofaulu kuanza kidato cha kwanza pia walioandikishwa kuanza
darasa la kwanza,” alisema. “Hata kama hana sare ya shule mvishe nguo
zake za nyumbani aende shule (na kumtafutia taratibu). Sio haki hata
kidogo kumkataza au kumzuia mtoto kwenda shule kwa sababu tu hana sare
kwani hilo sio kosa la mtoto,” alisisitiza Magalulla.
Aliwakumbusha wazazi na walezi kutambua kuwa kazi ya mtoto ni kusoma tu ambapo mzazi kazi yake ya msingi ni kumpelekea mtoto wake shule na kuhakikisha anahudhuria masomo na kumpa mahitaji mengine ya lazima.
Mkuu huyo wa mkoa pia amewaagiza maofisa elimu kuhakikisha watoto wanapokewa shuleni na kama kuna masharti hayajatimizwa basi wabaki wakiwadai wazazi kuyatimiza huku watoto wakiwa tayari wanaendelea na masomo.
“Pia ni wajibu wa wazazi na walezi ambao watoto wao wako shuleni wanasoma kushirikiana na walimu wao kuhakikisha kuwa kweli wanakwenda shuleni, maana baadhi ya watoto wanavaa sare lakini hawafiki shuleni, tuhakikishe watoto wana kwenda shule,” alisema.
Magalulla alisema ni kosa la kisheria kwa mzazi au mlezi kusababisha mtoto asiende shule au kumshawishi kukatiza masomo ili aweze kujihusisha na ajira.
Alionya kuwa mtu huyo akikamatwa atashtakiwa kwa sababu sheria inataka mtoto akianza shule lazima amalize. Kwa mujibu wa matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mkoa wa Rukwa mwaka jana, mkoa huo umefanya vibaya kwa kushika nafasi ya tatu kitaifa kutoka mwisho.
Halmashauri ya wilaya ya Kalambo ilishika nafasi ya 165 kati ya halmashauri 166 nchini.

No comments:
Post a Comment
paulmkale