Waziri wa
Kilimo, Mifugo na Uvuvi akiwasili kwenye mradi uliodumaa wa Ujenzi
wa machinjio ya kisasa wa ranchi ya Ruvu mapema hii leo. Sehemu ya jingo
lililobaki kama Gofu mara baada ya kutelekezwa na Uongozi wa Bodi ya
ranchi za Taifa(NARCO) Mwigulu Nchemba akishangaa namna mali hii ya Umma
ilivyotekelezwa.
Mwigulu Nchemba akiendelea kupewa maelezo ya kina kuhusu ubadhilifu uliojitokeza kwenye ujenzi huu.
Mh.
Ridhiwani kikwete Mbunge wa Chalinze akitoa malalamiko yake kwa Waziri
Mwigulu Nchemba kuhusu kukosekana kwa mahusiano mazuri kati ya wamiliki
wa ranchi na wananchi wanaozunguka ranchi ya Ruvu.
Kwa mbali
hili ndio jengo la machinjio ya kisasa lililokuwa linajengwa na hatimaye
kutelekezwa bila kuendelezwa tangu mwaka 2010.
Mwigulu
Nchemba akiteta jambo na viongozi wanaohusika na kulinda baadhi ya vifaa
vilivyonunuliwa kwaajili ya ranchi hiyo ya kisasa.(P.T)
Mh. Mwigulu Nchemba akioneshwa baadhi ya Ng’ombe wanaopatikana kwenye ranchi hiyo.
Mwigulu Nchemba akiwa kazini kwenye shamba la Mifugo la Ruvu hii leo.
Mwigulu Nchemba akidadisi utunzaji wa maji ya Mifugo inayopatikana ndani ya ranchi ya Ruvu.
…akipewa maelekezo
Mwigulu Nchemba
akiwa na Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani wakisikiliza kwa makini
sababu zilizopekea jingo hilo kutelekezwa.Anayetoa maelezo wa mwisho
kushoto ni msimamizi wa ranchi hiyo Ngd. Bwire.
Machinjio iliyotelekezwa
WAKATI
Taifa na Mataifa yakiendelea kutoa pongezi zao kwa serikali ya Rais.
J.P.Magufuli kwa speed yake ya kuchapa kazi, Mawaziri wake
pia wameendelea kuonesha namna walivyodhamiria kusimamia shughuli
za maendeleo ya Nchi yetu.
Hii leo,Mh:Mwigulu
Nchemba mwenye dhamana ya Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi amefanya
ziara ya siku moja kwenye ranchi ya Taifa ya Ruvu kukagua ujenzi wa
majengo ya machinjio ya kisasa ulioanza mwaka 2010.
Katika hali
ya kusikitisha na kulazimu kuchukua hatua za kinidhamu,Mwigulu Nchemba
amekutana na ubadhilifu wa Bilioni 5.7 ambazo zilitolewa kwaajili ya
ujenzi wa jengo hilo, Fedha hizo zilizokuwa zimelengwa kuwezesha ujenzi
wa machinjio hayo ya kisasa hazijafanya kazi kama ilivyokusidiwa.
Waziri huyo
wa kilimo amekuta mradi huo umetelekezwa tangu mwaka 2010
bila kuendelezwa, Sababu za kutelekezwa kwa mradi huo zikidaiwa kuwa
ni kutofautiana kwa mkandarasi na bodi ya NARCO (kampuni ya usimamizi
wa ranchi za Taifa) hazikukubalika na Mh:Mwigulu Nchemba ambaye baada
ya kusikiliza kwa makini ufafanuzi wa kutoka kwa viongozi wa ranchi
hiyo aliamua ifuatavyo.
Kwanza,
Mwigulu Nchemba amewatimua wakurugenzi wote wa bodi ya NARCO yenye
dhamana ya kusimamia ranchi za Taifa kwa kushinda kukamilisha ujenzi wa
mradi huo.Mbali na kushindwa,bodi hiyo imeutelekeza mradi huo na hivi
sasa inapendekeza kujengwa kwa mradi mwingine kama huo ndani ya eneo
hilohilo la ranchi ya ruvu.
Pili,
Mwigulu Nchemba amesitisha utumishi wa Mkurugenzi mkuu wa ranchi za
Tiafa kwa kushindwa kuchukua hatua za kusimamia ujenzi wa mradi huo
hadi kukamilika kwake.
Pia,
waziri huyo wa kilimo ameagiza kupitia vyombo vya sheria,wahusika
wote walioshiriki ama kwa makusudi au kwa njia yoyote kuhujumu mradi
huo usifanikiwe wanachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo.
Mwisho,
Nchemba amewaagiza wataalam wa wizara yake kuhakikisha ndani ya siku
7 wanampelekea ripoti ya thamani ya jengo lililokwisha kujengwa na
fedha zinazotakiwa kumalizia ujenzi wa jengo hilo.
Sambamba na
hatua hizo, Mwigulu ametoa rai kwa watumishi wote wa umma kuwa
mstari wa mbele kusimamia kwa ufanisi na uzalendo miradi yote ya
maendeleo ya nchi yetu, Mbali na hapo, serikali ya Magufuli haitakuwa
tayari kuona mali ya umma inachezewa na kuibiwa wakati kuna watanzania
wanaweza kusimamia mali hizo na kuziendeleza.
Picha/maelezo na Festo Sanga Jr.
No comments:
Post a Comment
paulmkale