Hawa Ndiyo ‘Maadui Wakubwa’ wa Diamond Kesho!



Diamond platinumz (11) 
Staa wa ngoma ya Utanipenda, Nasbu Abdul ‘Diamond’.
…’nayosema yana maana, sababu hakuna anayejua kesho, anayepanga ni Rabana, ila ameificha ni confidential, ukisali omba sana, mumeo nisije kuwa kichekesho, Maana rafiki wa jana, ndiye adui mkubwa keshoo!!!”
Ni mojawapo ya verse (ubeti) uliyomo kwenye hit single ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ’Diamond’ iitwayo Utanipenda? Wimbo ambao ndani ya takriban siku 30 tangu kuachiwa kwa video yake kwenye Mtandao wa YouTube umetizamwa karibu mara milioni 2!
Diamond platinumz (6)Moja ya vipande katika video mpya ya wimbo wa Diamond, Utanipenda
Katika wimbo huo, Diamond amejaribu kuvuta hisia na kujiweka katika nafasi ya msanii maarufu atakayefulia siku moja.
Amejaribu kuvuta picha na namna ambavyo mambo yanavyoweza kutokea kwake binafsi na kwa familia yake.
Ameenda mbele zaidi kuwazungumzia wadau wake wakubwa, au ‘marafiki zake’ katika mafanikio yake ya sasa namna ambavyo wanaweza kumgeuka, kwa sababu anatambua kwamba ‘rafiki wa jana, ndiye adui mkubwa kesho’
Katika Showbiz ya leo, nakuletea listi kamili ya ‘marafiki’ hao wanaoweza kuja kuwa ‘maadui wakubwa’ kesho ambao amewataja kwa majina mmojammoja na nguvu au mchango walionao katika maisha yake ya sasa na ya baadaye, japo hatuombei wala hatutarajii yamkute aliyoyawaza, lakini kama alivyosema mwenywewe ‘ Anayepanga ni Rabana, ila ameificha (kesho), ni confidential;
MENEJA TALE
Ametajwa kwenye vesi ya kwanza tu ya wimbo huo. Anajulikana kama , Hamis Tale ‘Babu Tale’ au Meneja Tale. Unaweza kusema ndiye Meneja Mkuu wa Diamond Platnumz.
Ni miongoni mwa wadau wakubwa vijana wa muziki nchini Tanzania, anasimamia na kuratibu karibu shoo zote za msanii huyu, ndani na nje ya Tanzania. Ndiye anayepokea michongo yote ya shoo za Daimond na kundi zima la Wasafi Classic Baby (WCB).
Katika wimbo huo, Diamond amemuweka katika kundi la meneja ambaye mambo yakiharibika, atakuwa hamtaki tena kiasi kwamba hata akimuona kwa mbali, atakuwa ana lala mbele (anamkimbia ni sheedah! Ameimba; Redio nyimbo wamezima, TV ndiyo hatari, meneja umebaki jina, hanitaki hata Tale…).
KIMWANA
Huyu ni dada wa hiyari wa Diamond, anajulikana zaidi kwa majina ya Halima Kimwana, ambaye amekuwa mtu wa karibu sana wa msanii huyo kiasi cha wengine kusema ni mpenzi wake ama dada yake damdam. Kutokana na ukaribu huo, bila shaka anajua mambo mengi ya Diamond na anaweza kuwa na athari katika maisha yake.
Diamond platinumz (9)Kutoka kushoto ni Sallam, Jackline Wolper, Babu Tale na God Father .
Kimwana ametajwa katika wimbo wa Utanipenda katika mstari mmoja wapo, pale Diamond anaposema “Kimwana sidadaangu, eti naye hanifahamu…” akimaanisha kwamba siku atakapofulia, Kimwana atajifanya hamfahamu licha ya ukaribu walionao sasa!
harmonizeHarmonize
HARMONIZE
Ni msanii chipukizi anayetamba na ‘hit singo’ ya Aiyola, majina yake ya kwenye paspoti ni Rajabu Abdulkhali a.k.a Harmonize. Kama Harmonize ana mtu anayemheshimu na kumthamini sana katika mafanikio aliyoyapata hadi sasa, basi ni Diamond, kwani ndiye msanii aliyetambua kipaji chake na kuamua kumsaidia kwa kumuweka chini ya lebo yake (WCB) na kuwa msanii wa kwanza kutolewa na kujulikana ndani ya muda mfupi.
Katika mabadiliko ya kimaisha anayoyatabiri Diamond katika Utanipenda, amemtaja msanii huyu kwa kusema;
“..Hata Harmonize nikimpigia ananifokea kama Sallam…..” akimaanisha kwamba hata huyu dogo atasahau wema wote aliomtendea mpaka kufanikiwa na kuanza kumletea nyodo kiasi cha kumfokea pale anapopigiwa simu ili amsaidie..dah!
SALLAM
Ni meneja wa Diamond akishirikiana na Babu Tale. Anajulikana kwa majina ya Sallam Sharaff ambaye ni mfanyabiashara, promota wa wasanii na mtendaji mkuu wa SK Entertainment. Ni kijana ambaye anamuongoza na kuendesha mambo mengi ya Diamond na ndiyo maana kwenye wimbo wake anamwambia Harmonise atakuwa akimfokea kama Sallam, kwani sasa hivi ndiye kama bosi wake pia.
Diamond platinumz (12)Kipande cha video hiyo kinachoonesha Mama Diamond akitimuliwa nyumbani kwa ‘JK’.
JK
Ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye Diamond anamuelezea kama ni mtu mwenye mchango mkubwa katika mafanikio yake, mbali ya kuwa ni kiongozi wa nchi, lakini kwake amekuwa mshauri na rafiki.
Hivyo katika hali ya kawaida, iwapo ikitokea Diamond akakwama, JK atakuwa mtu wa kwanza kumkimbilia kuomba msaada,lakini anaweza pia akajikuta anaishia getini na kufukuzwa.
Kwenye Video ya Wimbo wa Utanipenda, Diamond amemuonesha mama yake (Sandra) akiwa amembeba mgongoni mwanaye, Tiffah akienda kwa Jakaya kuomba msaada lakini anakataliwa na mlinzi hata kuingia ndani, anaishia getini.
FELLA
Jina lake kamili ni Said Fella, a.k.a Mkubwa Fella, ambaye hivi karibuni ameukwaa Udiwani wa Kata ya Mbagala jijini Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ni Meneja wa Yamoto Band, mvumbuaji na muendelezaji wa vipaji vya wasanii wa Bongo hasa vijana, ana kituo cha kuendeleza vipaji vya muziki wilayani Temeke.
Fella, Tale na Diamond wana masilahi ya pamoja katika Yamoto Band.
Fella naye ana ‘play part’ kubwa ya mafanikio ya Diamond na ndiyo maana ametajwa katika wimbo huo kuwa naye anaweza kuja kumgeuka baada ya kufulia ambapo mama yake anaonekana kweye video akienda kuomba msaada nyumbani kwa Mkubwa Fella lakini naye anaishia getini.
TIFFAH-DIAMOND.jpgDiamond akimbeba mwanaye, Tiffah
ROHO YAKE (TIFFAH)
Katika wimbo huu, Diamond anamtaja mtoto wake pekee, Princess Tiffah kama ndiye roho yake iwapo mambo  yataharibika.
Diamond anatuonesha namna ambavyo binti yake atahangaika. Tiffah ndiye mtoto wake wa kwanza na wa pekee hadi sasa, kwani tangu aanze uhusiano wa kimapenzi miaka kadhaa iliyopita na wanawake kadhaa, hakuwahi kupata mtoto.
Diamond platinumz (2)Diamond katika pozi na kimwana wake, Zari.
ZARI
Diamond ndiye ameshafulia, usupastaa hakuna tena, hapati shoo tena kama zamani na hata akipata hazijazi watu, kwake ni mikosi tu, sawa na jahazi kuzama. Swali linakwenda kwa mpenzi wake wa sasa, ambaye ni matawi ya juu na bila shaka amempenda
Diamond na kuamua kumzalia mtoto si kwa sababu ya pesa zake, bali pengine kwa umaarufu wake, kwa sababu ukilinganisha utajiri wa Diamond na wa Zari unaonesha Zari ni zaidi.
Katika wimbo huu, Diamond anamtupia swali mama watoto wake; Je, nawe utanipendaga au nawe ndiyo utanimwaga? (pindi atakapofulia).
MAADUI WENGINE
‘Maadui’ wengine watarajiwa wa Diamond ambao amewatajani pamoja na mashabiki zake, vyombo vya habari kama redio, TV na magazeti, amekwenda mbele zaidi kwa kuonesha ni magazeti gani ambayo atakapofulia na kumwagwa na Zari hayatasita kumuandika.
Kwenye video yake amelionesha gazeti hili la Ijumaa, gazeti namba moja la kuandika habari za mastaa nchini Tanzania, kuwa litakuwa na habari zake ukurasa wa mbele.
ANAUPENDA SANA
Kwa mujibu wa Diamond mwenyewe, wimbo huu wa Utanipenda ni wimbo ambao ametokea kuupenda zaidi kuliko nyimbo zake zingine kwa mwaka huu.
Sehemu au vesi anayoipenda zaidi ni hii inayosema: “…ooo bado nimewaza sana, zile tunzo, mashauzi ya airport, je itakapofika tamati, utadiriki hata japo kunipost?
Pindi shows zimekwama, nikipata sijazi ni mikosi, ooh jahazi limezama, Mola ninusuru baba.
“Kama namuona mwanangu, roho yangu, Tiffah Dangote, Anakwenda na Mama’ngu kwa Jakaya Kikwete wanafukuzwa watoke, usilie Sandra wangu, mboni yangu, jikaze usichoke….”
Nadiriki kusema Utanipenda ni miongoni mwa nyimbo zinazofundisha jamii na umewasilisha ipasavyo dhima ya msanii kwa jamii. Ni vyema kujua kuna maisha mengine kesho ambayo hatuyajui na tunatakiwa kujitambua katika hilo kadiri tunavyopata mafanikio.

No comments:

Post a Comment

paulmkale