Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Suleiman Jafo.
NAIBU
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Suleiman
Jafo, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauli ya Manispaa ya
Ilemela, John Wanga kutokana matumizi mabaya ya madaraka. Anaandika
Moses Mseti, Mwanza .
Naibu
huyo wa Tamisemi alitoa agizo hilo wakati akizungumza watumishi wa
manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, ambako amesema mkurugenzi huyo
ameshindwa kuhamia katika nyumba hiyo ambayo inakadiliwa kughalimu Sh.
200 milioni na kusababisha Serikali kuendelea kulipia nyumba anayoishi.
Amesema
kuwa licha ya Serikali kutoa agizo mkurugenzi huyo kuhamia katika nyumba
hiyo lakini yeye aliendelea kupangishia nyumba nzima inayolipiwa Sh. 2
milioni kwa mwezi licha ya kukamilika kwa nyumba iliyojengwa.(P.T)
Jafo
ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe CCM amesema kuwa katika manispaa hiyo
kuna matatizo mengi na kwamba itatumwa kikosi cha uchunguzi kutoka
Tamisemi ili kufanya uchunguzi namna ambavyo fedha za ujenzi wa uzio
zilivyotumika ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa watakaobainika kuhusika
na suala hilo.
“Huu
ukuta (uzio) hauwezi kughalimu fedha zote hizo, nyie hata kwa madai yenu
mnayosema mlifanya haraka kwa sababu ya uchaguzi sio kweli hamtaweza
kushawishi kwa hilo.
“Watanzania
wana shida, dawa hospitalini hakuna, wakina mama wanajifungulia chini
halafu, milioni 200 imekaa tu haina shughuli yeyote ile, mkurugenzi
unapaswa kupisha uchunguzi kufanyika kwanza,” amesema Jafo.
Hata
hivyo amesema kuwa ujenzi wa nyumba hiyo ulianza tangu mwaka 2013 lakini
mpaka sasa mkurugenzi huyo amekataa kwenda kuishi kwa sababu ya kuwa
chini ya kiwango na kwamba ipo katika maeneo hatarishi.
Pamoja na
kumsimisha Mkurugenzi huyo ametangaza kumsimamisha kazi Mhandisi wa
halmashauli hiyo, Jacob Nathaniel, pindi uchunguzi wa madai hayo
utakapoanza kuanzia katikati ya juma hili.
Hata
hivyo amesema licha ya uongozi wa manispaa hiyo kujipangia kiwango cha
Sh. 2 milioni kwa mwezi kipo juu ya kiwango cha serikali cha laki nane.
Kwa
upande wake mkurugenzi, Wanga katika kujitetea amesema sababu
zilizosababisha kushindwa kuhamia katika nyumba hiyo ni kutokana na kuwa
katika eneo hatarishi ikilinganishwa na nafasi yake ya ukurugenzi.
“Waziri
(Naibu Waziri Tamisemi) tunafanya kazi kubwa za wananchi na kazi zetu
mnazifahamu tunafanya watu wengine hawapendi tunachokifanya, sasa
nikihamia katika nyumba ile na ukilinganisha na eneo ilipo ni hatari,”
amesema Wanga.
No comments:
Post a Comment
paulmkale