Mbwa Kumtafuna Mbwa Mwenzake...!



Ndugu zangu,
Kwenye falsafa tunaambiwa, kuwa unapoletewa jambo kuna matatu ya kuyaangalia na kuyazingatia: Udadisi wa uhalisia wa jambo lenyewe (Reasoning), Mantiki ( Logic) na Ulinganishi wa nadharia ( Metafisiki)
Hivyo basi, unapokutana na mtu mzima mwenzako akakwambia, kuwa alipokuwa akitembea jana usiku, njiani alimwona mbwa akimtafuna mbwa mwenzake, basi, unachopaswa kufanya ni kutulia na kutafakari.
Yumkini usiku huo mtu huyo alikuwa akitoka kwenye kilabu cha pombe, na kwenye ulevi wake, paka aliyemwona akigombana na paka mwenzake, kwake ilikuwa ni mbwa anayemtafuna mbwa mwenzake! Tafakari.
Ni Neno Fupi La Usiku.
Maggid

No comments:

Post a Comment

paulmkale