Tukumbushane; Nwanko Kanu...
Ndugu zangu,
Nigeria ni kipenzi cha Waafrika, na Nigeria haikaukiwi vipaji.
Kila kwenye michuano mikubwa ya dunia, Nigeria ina historia ya kuja na wachezaji chipukizi wenye kufanya makubwa na kupata majina na hata kusajiliwa kwenye vilabu vikubwa.
Tunayakumbuka majina kama Sunday Oliseh, Julius Aghahowa, Emmanuel Amukise na mengine. Na mmoja nitakayemzungumzia hapa ni Nwankwo Kanu.
Baada ya kufanya vema kwenye Olimpiki Atlanta 1996, kiasi cha kutwaa dhahabu na hata kuwafunga Argentina, mwaka huo huo akatajwa kuwa mwanasoka bora Afrika.
Na mafanikio hayo yakamfanya asajiliwe na Ajax Amsterdam na baadae Inter. Akiwa Inter madaktari wakabaini kuwa Nwanko Kanu ana tatizo la moyo la tangu kuzaliwa.
Wapenzi wa soka tukakata tamaa tukidhani kuwa Nwankwo Kanu asingerudi tena uwanjani. Hata hivyo, madaktari bingwa walimfanyia operesheni ya moyo iliyofanikiwa sana na hata kumaliza tatizo lake.
April 1997 Kanu alirudi tena uwanjani akiwa bora zaidi kimpira. Mwaka 1999 alihama Inter akaenda kucheza Uingereza na vilabu vya Arsenal, West Bromwich na Portsmouth.
Kwa sasa Kanu ni balozi wa Unicef na ana mfuko wake mwenyewe- Kanu Heart Foundation kwa ajili ya kutoa huduma kwa watoto wa Afrika waliozaliwa na matatizo ya moyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
paulmkale