Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais
Mstaafu wa Awamu ya tatu, Mh. Benjamini William Mkapa, Ikulu jijini Dar
es Salaam leo January 7,2016.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamini William Mkapa, Ikulu jijini Dar
es Salaam alipomtembelea leo.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es
Salaam leo January 7,2016.(P.T)
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar
es Salaam alipomtembelea leo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es
Salaam baada ya kufanya mazungumzo January 7,2016
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe
07 Januari, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa
awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu
Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu Jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara
baada ya Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Mkapa amesema lengo la kukutana
na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na watanzania
kuiongoza nchi, kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.
Rais Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari
kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika
kufanya hivyo.
Kwa upande
wake Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na
kumtakia heri ya Mwaka Mpya, amempongeza Rais Magufuli kwa jinsi
alivyoanza kazi vizuri hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato,
kubana matumizi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo
yanawahusu wananchi yakiwemo afya na maji. Jaji Warioba ameongeza kuwa
Watanzania wote wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi kubwa
anazofanya, ambazo ni kukomesha rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya
madaraka na wizi wa mali ya umma.
“Lazima kila
mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachie, pale ulipo kama ni mambo
ya rushwa uanzie hapo hapo, kama ni mambo ya matumizi mabaya ya madaraka
anzia hapohapo, tusije tukamuachia Rais pekee yake, yeye awe kiongozi
wetu, lakini watanzania wote tushughulike na matatizo hayo” alisisitiza
Jaji Warioba.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,
IKULU Dar es salaam
No comments:
Post a Comment
paulmkale