SERIKALI: TUNA IMANI MBWANA SAMATTA ATASHINDA TUZO LEO USIKU


Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Daniel Ole Njoolay amesema ana imani kubwa Mtanzania, Mbwana Samatta atashinda tuzo ya Mwasoka Bora Afrika.

Samatta anawania tuzo ya mwanasoka bora Afrika kwa wale wanaocheza soka ndani ya bara hilo. 
Njoolay amezungumza na Radio One na kuiambia Samatta amewasili  salama na wana matumaini makubwa atafanya vizuri.


OLE NJOOLAY

"Amewasili hapa jana saa saba, tumempokea, anaonyesha ni mwenye furaha na kwa kweli tuna matumaini atafanya vizuri," alisema Njoolay.

Samatta ameingia fainali na kipa mkongwe wa TP Mazembe, Muteba Kadiaba na mshambuliaji wa Etoile Du Sahel, Bouned Baghdad raia wa Algeria.


Matumaini ya Afrika mashariki yamo kwenye kitengo cha tuzo ya mchezaji bora anayechea soka barani Afrika ambapo mshambuliaji Mbwana Aly Samatta wa Tanzania na klabu ya TP Mazembe yumo ndani.
Nyota huyo aliyeisaidia klabu ya Mazembe kuondoka na kombe la klabu bingwa afrika, atakuwa anawania taji hilo dhidi ya mdakaji wa klabu yake ya Mazembe, Robert Kidiaba ambaye pia ni kipa wa DR Congo na raia wa Algeria Baghdad Bounedjah anayeichezea Etoile du Sahel.
Samatta aliibuka mfungaji mabao bora Ligi ya Klabu Bingwa Afrika mwaka uliopita.
Katika kitengo cha Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kinachoshirikisha wachezaji wa ligi za nje, Yaya Toure, aliyeshinda tuzo hiyo mara nne awali, ni mmoja wa wanaoipigania.
Toure, ambaye ni kiungo wa Ivory Coast na Manchester City anakabiliwa na upinzani kutoka kwa mshambuliaji wa Gabon na klabu ya Borrussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang, na Andrew Ayew kutoka Ghana na Swansea City.
Tangu kuanzishwa kwa tuzo hizo 1992, ni wachezaji kumi na wanne pekee wakiwemo Yaya Toure na Didier Drogba ambao wametuzwa.
Image caption Toure aliongoza Ivory Coast kutwaa ubingwa wa Afrika mapema 2015
Wanamuziki maarufu akiwemo Awilo Longomba, watatoa burudani katika hafla hiyo inayotarajiowa kuhudhuriwa na mamia ya wachezaji, wasimamizi na wapenzi wa soka.
Mchezaji bora wa kike pia atapatikana kati ya orodha inayojumuisha raia wa Cameroon Gabrielle Onguene na Gaelle Enganamouit, Ngozi Ebere wa Nigeria, N’rehy Tia Ines wa Cote d’Ivoire na Portia Boakye kutoka Ghana.
Wachezaji wa umri mdogo
  • Adama Traore - Mali,
  • Kelechi Nwakali - Nigeria,
  • Samuel Diarra - Mali,
  • Victor Osimhen - Nigeria
  • Yaw Yeboha - Ghana
Kocha Bora
  • Baye Ba –Mali
  • Emmanuel Amuneke – Nigeria
  • Fawzi Benzarti - Etoile Sportive de Sahel,
  • Herve Renard - Cote dIvoire
  • Patrice Carteron - TPMazembe
Wachezaji wanaoibuka
  • Azubuike Okechukwu - Nigeria,
  • Djigui Diarra - Mali
  • Etebo Oghenekaro - Nigeria,
  • Mahmoud Abdelmonem - Misri
  • Zinedine Ferhat - Algeria
Tuzo za wakongwe
  • Charles Kumi Gyamfi – Ghana
  • Samuel Mbappe Leppe - Cameroon
Timu Bora ya Taifa ya mwaka
  • Ivory Coast
  • Ghana
  • Mali U-17
  • Nigeria U-17
  • Nigeria U-23

No comments:

Post a Comment

paulmkale