Msafara
wa Naibu Waziri Nishati na Madini, Dk.Medard Kalemani ukikagua ujenzi wa
kituo kipya cha mjini Singida cha kutawanya umeme kilovoti 400 wa gridi
kutoka nchini Kenya na Tanzania. Kituo hicho kitasambaza umeme kutoka
Singida kwenda mkoa wa Iringa na Shinyanga.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dk.Medard Kalemani (wa kwanza kushoto
mwenye miwani) akizungumza na maafisa kutoka ofisi na madini kanda ya
kati mkoa wa Singida na wa wilaya ya Manyoni, kwenye ofisi ya Mkuu wa
wa wilaya hiyo ya Manyoni Fatma Touefiq.Wa pili kushoto ni Afisa Madini
kutoka osifi ya madini kanda ya kati ambaye jina lake halikufahamika
mara moja, Kamishina msaidizi wa madini kanda ya kati, Sosthenes Massola
na Meneja wa kampuni ya Spencon inayosambaza umeme (REA) vijiji vya
mkoa wa Singida, Machil Rao.
Naibu
Waziri Nishati na Madini, Dk.Medard Kalemani (katikati mwenye miwani)
akisisitiza jambo kwa wamiliki wa migodi ya madini ya Gypum iliyopo
kwenye kijiji cha Itigi wilayani Manyoni, Ismael Ivata Kushoto) na
Yusuph Kibira (kulia mbele).
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dk.Medard Kalemani (wa pili kushoto)
akichunguza madini ya gypum maji inayotukika kutengenezea chaki katika
kiwanda kidogo cha Mukhtar Mahamoud kijiji cha Itigi wilaya ya Manyoni.
Dk.Kalemani ameahidi kushirikiana na mamlaka mbalimbali kutafuta soko la
uhakika la chaki zinazotengenezwa na viwanda vidogo cha chaki Itigi.Wa
tatu kushoto ni mbunge wa jimbo la Singida magharibi (CCM) Yahaya
Masare.(P.T)
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Dk.Medard Kalemani, (mwenye miwani) akipewa
maelezo juu ya chaki zinazotengenezwa na kiwanda kidogo ya Mukhtar
Mahamoud cha kijiji cha Itigi wilayani Manyoni.
Lori
likiwa limepakia madini aina ya Gypsum yanayochimbwa katika kijiji cha
Itigi, kwa ajili ya kusafirisha kwenda nchini Rwanda.(Picha zote na
Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Manyoni
Serikali
imeingiza Kampuni ya Spencon ya jijini Nairobi, Kenya, kumaliza kazi ya
usambazaji umeme katika vijiji 73 vya mkoa wa Singida ambavyo bado
havijapata umeme wa (REA) kabla ya Mei mwaka huu.
Endapo
kampuni hiyo itashindwa kumaliza kazi katika kipindi hicho
itanyang’anywa vifaa vyake, ili kufidia hasara itayotokana na kuchelewa
kumaliza kazi kwa mujibu wa matakwa ya mkataba.
Hayo
yalisemwa juzi na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard
Kalemani,muda mfupi baada ya kukagua kazi ya usambazaji wa umeme kupitia
mradi wa REA 11 katika kijiji cha Heka wilayani Manyoni mkoa wa
Singida.
Alisema
kwa mujibu wa mkataba wa serikali na kampuni Spencon, kazi ya usambazaji
wa umeme iliyoanza Oktoba 2013 katika vijiji 90 vya mkoa wa Singida,
ilitarajiwa kuwa imemalizika Novemba mwaka jana lakini hadi sasa ni
vijiji 17 pekee ndio vilivyopata umeme huo.
“Serikali
imelipa kampuni ya Spencon malipo yake yote, kwa sasa haina sababu ya
kuendelea kuvumilia wananchi wasipate nishati hii ya umeme kwa maendeleo
yao. Nakuagiza meneja wa TANESCO Mkoa wa Singida, simamia kazi hii
usiku na mchana ili vijiji vyote vilivyopo kwenye mradi wa REA II, viwe
vimepata umeme kabla ya Mei mwaka huu,” alisema.
Aidha
Naibu Waziri huyo, ameiagiza Kampuni ya Hainan International Limited ya
nchini Korea, inayojenga kituo mbadala mjini cha kusambaza umeme wa
Kilovoti 400, kumaliza kazi hiyo ndani ya muda uliowekwa kwenye mkataba.
Dkt.
Kalemani alisema kazi hiyo ya kuunganisha umeme wa gridi kutoka nchini
Kenya na wa nchini na kisha umeme huo kusambazwa hadi mikoa ya Iringa na
Shinyanga na hatua hiyo itasaidia kurahisisha utekelezaji wa ahadi ya
serikali ya awamu ya tano ambayo iliahidi kuifanya Tanzania kuwa nchi ya
viwanda.
Katika
hatua nyingine Naibu Waziri huyo, aliwataka wachimbani wa madini
mbalimbali wadogo, wajiunge au waanzishe vikundi na kuvisajili kisheria,
ili serikali iweze kuwapatia ruzuku kuboresha shughuli zao.
“Serikali
ya awamu ya tano, inatambua na inathamini shughuli zinazofanywa na
wachimbaji madini wadogo, wakati na wale wakubwa, sababu kuu ikiwa ni
kwamba sekta hiyo ina fursa nyingi za ajira na pia inapatia
mapato(mrahaba) kwa maendeleo ya nchi,” alisema Naibu Waziri..
Alisema
kwa hali hiyo,serikali kuu itaendelea kuboresha mazingira ya kufanyia
kazi na kwa wachimbaji na kutoa ruzuku kwa vikundi vitakavyokidhi
vigezo.
Dkt.
Kalemani pia amewakumbusha wachimbaji hao, kutunza mazingira katika
maeneo wanayochimba madini kwa kupanda miti na kufukia mashimo baada ya
kumaliza kuchimba madini.
Aidha
Naibu Waziri aliahidi viwanda vidogo vya kutengeneza chaki mkoani
Singida kuwa Wizara ya Nishati na Madini itashirikiana na Wizara ya
Elimu na Ufundi kuwasaidia kutafuta soko la biashara zao ili waweze
kunufaika na kazi wanayoifanya.
No comments:
Post a Comment
paulmkale