1. TRA yakusanya trilioni 1.4 kwa mwezi Desemba..
Hii ni
habari kubwa inayopewa nafasi ya kwanza na mtandao wa.
Inahusu pato la taifa. TRA inaelekea kufanya kazi njema na ya kupongezwa
katika kukusanya mapato ya taifa. Kodi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
2. Magufuli kukabidhiwa CCM Juni
Habari
hii inachukua nafasi ya pili kwa ukubwa. CCM ni chama tawala. Uenyekiti
wa CCM ni nafasi muhimu. Ni jambo jemba jema Mwenyekiti wa sasa na Rais
Mstaafu ameamua kumpa nguvu zaidi Rais Magufuli kwa kumwachia Uenyekiti
CCM.
3. Chadema wakutana
Chama Cha
Demokrasia Na Maendeleo- Chadema, ni chama kikuu cha upinzani. Taarifa
za Chadema kukutana Moshi zimevuta macho na masikio ya wengi. Bila
shaka, baada ya uchaguzi mkuu, Chadema wanakutana kujipanga, na kutakuja
na tamko au matamko yatakayotokana na vikao hivyo. Hii ni habari ya
tatu kwa ukubwa leo.
Soma habari nyingine za ndani ikiwamo katuni bora ya leo.
No comments:
Post a Comment
paulmkale