Baadhi ya mitambo iliyotelekezwa kwenye Kiwanda cha kutengenezea Zana za Kilimo ZZK
Mitambo ambayo ilikuwa ikitumika kutengenezea Zana za Kilimo katika kiwanda cha ZZK Iyunga jijini Mbeya ikiwa imetelekezwa
Niranjan
Bandi, aliyejitambulisha kuwa ndiye Mkurugenzi mkuu wa shughuli
zinazoendelea katika kiwanda cha ZZK chini ya kampuni ya CMG akiwapa
maelezo waandishi wa habari.
Waandishi wakitoka katika kiwanda cha ZZK huku wakijiuliza maswali mbali mbali kutokana na walichokikuta ndani ya kiwanda hicho.(P.T)
Baadhi ya
waandishi wakichungulia ndani ya majengo ya kilichokuwa kiwanda cha
kutengeneza sabuni HISOAP Kushuhudia kama kuna kilichosalia.
Huu ndiyo
muonekano wa ndani ya majengo ya kilichokuwa kiwanda cha kutengenezea
sabuni HISOAP kukiwa hakuna kitu licha ya kuwepo Mlinzi
Muonekano wa Jengo la kiwanda cha HISOAP lililotelekezwa ili hali serikali ya awamu ya tano ikisisitiza kuwa serikali ya Viwanda CHAMA
Cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) katika
kutekeleza majukumu yake kimefanya ziara katika viwanda vine vilivyopo
Iyunga jijini Mbeya na kushuhudia baadhi vikiwa vimetelekezwa.
Waandishi hao 15 kutoka vyombo mbali mbali ambao ni wanachama wa TAJATI, walifanya ziara hiyo iliyoanzia
katika majengo yaliyokuwa ya Kiwanda cha kutengenezea sabuni
kilichokuwa kikijulikana kwa jina la HISOAP kilichopo Iyunga jijini
Mbeya na kukutana na majengo hayo yakiwa yametelekezwa.
Mbali na kutelekezwa kwa majengo hayo,pamoja na kuwepo
kwa mlinzi ambaye alikiri kulinda majengo ambayo ndani yake hajui
kilichomo kwa kupitia matundu ya mlangoni,wanahabari hao walishuhudia
ndani kukiwa hakuna hata mtambo mmoja ulichosalia na na matanki makubwa
yanayoendelea kuoza nje.
“Mimi
nalinda hapa kwa maagizo ya bosi wangu lakini huko ndani hakuna
shughulli yoyote inayofanyika kwani hata hizo mboga zilizolimwa ni mali
ya walinzi wenzetu ndiyo wamelima,sijui humo ndani kama kuna mitambo
sijawahi kuona milango ikifunguliwa hata mwenye funguo simjui” alisema
Mlinzi ambaye alitaka jina lake lihifadhiwe kwa usalama wake.
Aidha
katika ziara hiyo timu ya waandishi ilifika katika majengo ya
kilichokuwa kiwanda cha serikali, Kiwanda cha kutengenezea zana za
kilimo maarufu kwa jina la ZZK ambapo timu hiyo ilipokelewa na raia
mmoja wa kigeni mwenye asili ya kiasia, Niranjan Bandi, aliyejitambulisha kuwa ndiye Mkurugenzi mkuu wa shughuli zinazoendelea hapo chini ya kampuni ya CMG.
Katika
maelezo yake kwa waandishi wa habari Bandi alisema ndani ya kiwanda
hicho kuna shughuli za kutengeneza vipuri vya magari, uunganishaji wa
matrekta madogo ya kilimo(powertiller ) kutoka China na kwamba zana za
kilimo wameshindwa kutengeneza kutokana uchakavu wa mitambo iliyopo na
imepitwa na teknolojia.
Aliongeza
kuwa ifikapo januari 15 mwaka huu wanatarajia kuanza kutengeneza mabati
baada ya kupata mtambo kutoka China ambao hivi sasa unafanyiwa
marekebisho kabla ya kuanza kazi sambamba na uanzishwaji wa kiwanda cha
kuzalisha bia cha Serengeti.
Wakati mwekezaji huyo akijieleza na kuonyesha mashaka makubwa ya uzalishaji kuwa ni changa la macho,Waandishi wa habari walishuhudia
mitambo iliyokuwa ya kutengenezea zana za kilimo ikiwa imetekelezwa
bila kufanya kazi ndani ya majengo hayo ambapo Mkurugenzi huyo alisema
hawana uwezo wa kuiendesha.
Baada
ya kukamilisha mahojiano na Mkurugenzi huyo waandishi hao walielekea
moja kwa moja katika kiwanda cha Malumalu cha Marmo Granito ambapo
walitembelea mitambo ya kuchonga na kukata mawe na bidhaa mbali mbali
zinazotokana na miamba ya asili.
Mkurugenzi
wa Marmo,Salim Jessa alisema tangu walipoanza uwekezaji katika Mkoa wa
Mbeya wameanza kupata masoko nje ya nchi ikiwemo India,Italia na
kutafuta masoko mengine nchini China ambako watakuwa wakiuza malighafi zilizoongezwa thamani kwa ajili ya matumizi mengine.
Alisema
changamoto kubwa ni ushindani wa soko baada ya kampuni zingine
kujitokeza na kuanza kutengeneza bidhaa zinazotokana na mawe ya asili
kama wao sambamba na uingizaji wa bidhaa zilizochakachuliwa kutoka nje
kwa lengo la kuharibu soko.
Ziara
hiyo ya TAJATI ilihitimishwa katika kiwanda cha Bia cha TBL ambapo
waandishi walitembezwa kiwandani hapo na kisha kupata muda wa kuuliza
maswali kutoka kwa wahusika.
Akizungumza
na wanachama hao, Meneja wa Kiwanda cha Bia Mbeya, Waziri Jemedari
alisema licha ya mafanikio waliyoyapata katika uzalishaji wanakabiliwa
na changamoto kubwa ambazo ni miundombinu mibovu, gharama kubwa za maji
na umeme sambamba na mlundikano wa vinywaji kutoka nje ya nchi
vinavyoharibu bei ya vinywaji vinavyozalishwa nchini.
Jemedari
alisema bia nyingi zinaingizwa nchini kutoka nje zinauzwa bei ya chini
hivyo kupelekea wateja wengi kukimbilia na kuua soko la vinywaji vya
ndani.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment
paulmkale