Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeiagiza Idara ya Uhamiaji nchini kuanza Operesheni maalum ya kuwabaini wageni walioingia na kufanya kazi ambazo sio za kitaalamu zinazoweza kufanywa na Watanzania ili kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwaondosha.
Agizo
hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad
Masauni baada ya kutembelea Makao Makuu ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar
Es Salaam na kuzungumza na makamishna wa idara hiyo.
Akiwa
katika ofisi hizo kukagua shughuli zinazoendelea kwenye idara hiyo,
Naibu waziri huyo amesema, kumekuwa na ongezeko kubwa la wageni wasikuwa
na tija katika nchi ambao wengi wao wamekuja na kuomba vibali vya
uwekezaji au kazi za kitaalam badala yake wamekuwa wakifanya kazi na
biashara ambazo Watanzania wa kawaida wanaweza kuzifanya.
Afisa
Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Johannes Msumule
akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Yussuf Masauni alizungumzia hatua
zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti wageni wanaoishi na kufanya kazi
nchini kinyume na sheria. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam
Sehemu
ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhe. Hamad Yussuf Masauni, wakati wa mkutano wa kuzungumzia hatua
zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti wageni wanaoishi nchini na kufanya
kazi kinyume na sheria. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
paulmkale