“Nimerekodi kazi na Chameleone,itafanyiwa final mixing nchini Uganda na producer wake, jina la wimbo sita weka wazi sasa ila wimbo nimeandika sehemu yangu na Chameleone ameandika yake,Utatoka mwezi wa kumi mwaka huu”. Amesema Bob Junior.
Ameongeza kuwa anatarajia kwenda Uganda kuikamilisha kazi hiyo.
“Naenda Uganda wiki ijayo kuikamilisha kazi na sijamlipa Chameleone pesa yeyote ila tutafanya kazi kwa mkataba kuanzia sasa, sisi ni Business Partners”.
Wiki iliyopita Chamelione alikuwepo Tanzania ambapo alifanya show Club Maisha ya Dar es salaam siku ya Ijumaa na kesho yake Jumamosi alikinukisha Dodoma.
No comments:
Post a Comment
paulmkale