Showing posts with label NEWS. Show all posts
Showing posts with label NEWS. Show all posts

Dont miss the secret of this successful marriage between jessica nkosi and tk dlamin with their sibling

Jessica made the announcement on Instagram on Friday by sharing the cutest picture of her little family. 
The proud mama also revealed that their little girl's name is Namisa 'Nami' Dlamini. 
"I love this girl with a love I can’t even begin to describe. I’m so blessed, I’m so in love. It’s been a month of pure bliss. This little star has stolen my heart." 
After months of speculation Jessica first revealed that she was expecting on the cover of True Love magazine in June.
The fiercely private star said she decided to keep her pregnancy away from the spotlight until she was ready because she didn't want it to be linked to any drama. 
"There's nothing scandalous about my pregnancy. Therefore, I don't want any drama around it and I certainly don't want anyone to have an opinion about it."


A VIDEO YOU MUST WATCH, WATCH HERE

Breaking News: New Story In Town Big Snake In Trouble

BREAKING NEWS: Lugola Ampa Maagizo Mazito IGP Sirro Kuhusu Sakata la Lugumi.......Pia Kamtaka Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Kufika Ofisini Kwake July 25

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Simon Sirro kumpeleka ofisini kwake mmiliki wa kampuni ya Lugumi, Said Lugumi.

Amesema Lugumi anatakiwa kufika katika ofisi yake iliyopo mjini Dodoma Julai 31, 2018 saa 2 asubuhi.

“Waliopita hawakuwa maninja sasa ameingia ninja namtaka Lugumi aje muda ukifika tutawaambia Watanzania,” amesema.

Waziri Lugola ametoa kauli hiyo leo  mbele ya waandishi wa habari alipokuwa akitoa tathmini ya ziara aliyoifanya kuanzia Julai 11, 2018  kwenye taasisi mbalimbali zilizo chini ya wizara yake.

Pia amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida),  Andrew Massawe kufika ofisini kwake Julai 25, 2018 mjini Dodoma akiwa na mtambo wa kutengeneza vitambulisho vyaTaifa au kampuni ikiwa na fedha hizo.

Amesema kuna kampuni iliyopewa jukumu la kuleta mtambo kwa ajili ya vitambulisho hivyo  na muda umeisha bila mtambo huo kuonekana.

“Afike ofisini kwangu mjini Dodoma pamoja na watu waliopewa tenda hiyo waje na mtambo au fedha hizo kiasi cha Sh32 bilioni,”amesema Lugola.

Amesema watu hao kama hawana fedha  au mtambo basi wawe na maelezo yatakayojitosheleza kwa nini mtambo huo haujawasili hadi leo.
==

BREAKING NEWS : Nyalandu arudi CCM rasmi leo hii

Aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu amejikuta kwenye majibizano na baadhi ya wafuasi wake kwenye mtandao wa kijamii wa twita  baada ya kuambiwa arudishe twiga (Bila kufafanuliwa ni twiga yupi).

Majibizano hayo yaliibuka ikiwa ni muda mfupi  baada Mh. Nyalandu kuweka maneno yakutia ujasiri, na ya ushauri wa kutokata tamaa na baada ya maoni akafikia hatua ya kumjibu mfuasi mmoja kwa kumfananisha na watu waliolaaniwa.

Mfuasi huyo aliyekwenda kwa jina la 'Tamankila1' katika mtandao wa Twitta alimwambia Nyalandu kwamba anapaswa kurudisha Twiga ili aweze kueleweka, huku mfuasi mwingine akimwambia kwamba neno moja kwenye biblia ndilo litakalomuokoa ambalo ni lile la "Mimi sikuja kwa wenye haki bali kwa waovu".

"Tamankila1 watu kama wewe wamelaaniwa. Huwezi kuanza siku kwa kusema uongo ili ujisikie umesomeka kwenye mitandao ya kijamii. Ni twiga yupi unayetaka nimrudishe, na nilimchukua wapi. Imeandikwa, waongo wote, sehemu yao ni katika ziwa liwakalo kwa kiberiti" Ujumbe wa Nyalandu kwa mmoja wa wafuasi wake..

Majibizano hayo ambayo bado yameendelea kwenye ukurasa wa Twitta yalitokana na  ujumbe wa  Mh. Nyalandu unaosema;  "Ukweli katika maisha ni huu, kwamba Mungu hakuachi. Amini katika uwezo na ukuu wake. Ujapopita katika changamoto zozote katika maisha, hata wale wa karibu nawe wakikuacha, Yeye ni Amini na Kweli, hatakuacha, atakupigania, na atakufanya heri kwa ajili ya utukufu wake"

Tangu alipojiuzulu nafasi ya ubunge wa Singida Kaskazini, Oktoba 30, 2017,  Mh. Nyalandu amekuwa akiandamwa na skendo za kuuza vitalu pamoja na twiga ambapo aliweka wazi kuwa yupo tayari kujibu tuhuma hizo kwa kuwa anajiamini aliitumikia wizara hiyo kwa uaminifu mwaka 2014 - 2015.

Baada ya tuhuma hizo akiwa nje ya uongozi, Nyalandu aliwahi kumjibu Waziri wa Maliasili na utalii wa sasa Dk. Hamisi Kigwangalla kwamba anasikitika sana kuona Waziri huyo akitumia muda wake ndani ya Bunge kumchafua na kumdhihaki ilihali alifanya mambo makubwa ndani ya wizara hiyo ikiwa kupambana na ujangili kwa kiasi kikubwa.

==>>Ujumbe wa Nyalandu uliozua majibizano mtandaoni

==

BREAKING NEWS: Zahanati Yateketea Kwa Moto....Mtendaji wa Kijiji Mbaroni Kwa Mahojiano

Watu watano akiwamo ofisa mtendaji wa kijiji cha Ulaya, wilayani Igunga mkoani hapa,  Zablon Hussin wanashikiliwa polisi kwa mahojiano wakihusishwa na tukio la jengo la zahanati ya kijiji hicho kuungua moto.

Jengo hilo liliungua moto usiku wa Julai 14, 2018 na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh85 milioni.

Akizungumza na wanahabari leo Jumamosi Julai 21, 2018  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema majina ya watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa yanahifadhiwa kuepuka kuharibu upelelezi.

"Wakati moto huo unazuka, zahanati ile haikuwa na mlinzi na tayari tumetoa maelekezo kwa viongozi wa Serikali za mitaani kuhakikisha maeneo yote ya umma yanakuwa na ulinzi," amesema Kamanda Nley.

Kaimu Mganga Mkuu wilaya ya Igunga, Dk Bonaventura Kalumbete amesema moto huo pia umeteketeza dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya Sh25 milioni.

Dk Kalumbete amesema juhudi zinaendelea kutafuta jengo jingine ili litumike kwa ajili ya huduma wakati mchakato wa ukarabati zahanati iliyoungua ukiendelea.

Breaking News: Wema Sepetu ahukumiwa jela mwaka mmoja kwa Madawa ya Kulevya

Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya milioni 2 baada ya kukutwa na makosa mawili ya kutumia na kuhifadhi dawa za kulevya aina ya Bangi nyumbani kwake.

Akisomewa hukumu hiyo leo Julai 20, 2018 katika Makahama ya Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam, Wema Sepetu ametakiwa kulipa faini hiyo na kama akishindwa basi atapelekwa jela kutumikia adhabu hiyo.

Katika hukumu nyingine wafanyakazi wawili wa ndani wa msanii huyo ambao nao walitajwa kwenye kesi hiyo wameachiwa huru na mahakama hiyo kwa kukutwa bila hatia.
==

Breaking News: NECTA Yatangaza Matokeo ya Kidato cha Sita 2018.....Bofya Hapa Kuyatazama

Baraza la Mtihani la Tanzania (NECTA) limezuia matokeo ya watahiniwa kumi na tatu kutokana na sababu kadhaa na wengine nane kufutiwa kabisa matokeo kwa sababu ya udanganyifu.

Akitaja sababu za kuzuiwa kwa matokeo hayo, Katibu mtendaji wa baraza hilo Dkt. Charles Msonde wakati akitangaza matokeo hayo leo visiwani Zanzibar, amesema kuwa kuna baadhi ya watahiniwa walishindwa kukamilisha mitihani yao kutokana na sababu za kiafya na hivyo kufanya mitihani nusu, watapewa nafasi ya kurudia mwaka unaofuata.

Licha ya hiyo, Dkt. Msonde amesema kuwa ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 96.06% mwaka 2017 hadi 97.12% mwaka huu, huku ufaulu katika masomo ya sayansi umeshuka ukilinganishwa na masomo ya sanaa na biashara.

“Jumla ya watahiniwa 83,581 sawa na asilimia 97.58 ya watahiniwa waliofanya mitihani ya kidato cha sita Mei mwaka huu wamefaulu huku wasichana wakiwa ni 34,358, na wavulana waliofaulu ni 49,223 pekee”, amesema Dkt. Msonde.

Dkt. Msonde ameongeza kuwa tathmini ya hali ya matokeo imeonesha kuimarika kwa ufaulu katika madaraja ya I,II na III ikiwemo kupanda kwa asilimia 1.80 kutoka 93.72 mwaka 2017 na kuwa asilimia 95.52 mwaka 2018.

Shule zilizofanya vizuri zimetajwa kuwa ni Kibaha, Kisimiri, Kemebos na Mzumbe, Feza Boys, Marian Boys, AHMES, St Mary's Mazinde Juu, Marian Girls & Feza Girls.

Kuona matokeo ya Kidato cha Sita 2018 <<BOFYA HAPA>
==

FORM SIX NATIOANAL EXAMINATION RESULTS (ACSEE RESULTS 2018) | Matokeo Kidato Cha Sita 2018

FORM SIX NATIOANAL EXAMINATION RESULTS (ACSEE RESULTS 2018)

Kauli ya Sumaye ya Kwamba Alienda Upinzani Kwa Faida ya CCM Yawachanganya Wengi


"Nimeenda upinzani kwa maslahi ya nchi hii na kwa faida ya CCM"- kauli aliyoitoa Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Sumaye mbele ya Rais Magufuli jana walipokutana viongozi wote wastaafu.

Watu mbali mbali wamekua wakihoji kauli hiyo Ina maanisha nini

Breaking News: Sumaye Karudi CCM rasmi leo hii katangazwa


"Nimeenda upinzani kwa maslahi ya nchi hii na kwa faida ya CCM"- kauli aliyoitoa Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Sumaye mbele ya Rais Magufuli jana walipokutana viongozi wote wastaafu.

Watu mbali mbali wamekua wakihoji kauli hiyo Ina maanisha nini

Nape Nnauye Kalianzisha Tena Huko Twitter.......‘Watashindana lakini hawatashinda’.

Ujumbe wa mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye katika akaunti yake ya Twitter, umeibua mjadala kuanzia jana hadi leo.

Katika mjadala Nape hakuwa nyuma katika kujibizana na wafuasi wake wanaomuunga mkono huku wengine wakimkosoa.

Jana Nape alituma ujumbe ulioambatana na picha ya simba, kisha akaandika,‘Watashindana lakini hawatashinda’.

Katika picha hiyo, pia aliambatanisha kifungu cha Biblia kutoka Daniel 6:16 kinachosema: “Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Daniel, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena akamwambia Daniel, Mungu wako unayemtumikia, daima yeye atakuponya.”

Dakika chache tu baada ya kutuma ujumbe huo, wafuasi wake walianza kumponda huku wengine wakimuunga mkono.

Baada ya Kutumbuliwa Mwigulu Aongea Haya Kuhusiana na Kifo cha Maji Marefu

Baada ya Kutumbuliwa Mwigulu Aongea Haya Kuhusiana na Kifo cha Maji Marefu
Kufuatia kifo cha Mbunge wa Korogwe vijijini (CCM), Stephen Ngonyani almaarufu kama Profesa Maji Marefu kilichotokea usiku wa jana, kimemuibua aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Mwigulu ambaye amevuliwa uwaziri na Rais Magufuli wikiendi iliyopita amesema kuwa CCM imepata pigo kwa kumpoteza kada na kiongozi wa kweli.

“Maandiko matakatifu yanasema, Mwanadamu aliyezaliwa na Mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, Tumempoteza kaka,ndugu na rafiki Comrade Stephen Hilary Ngonyani (Prof.MajiMarefu), tumempoteza Kiongozi na kada kweli kweli wa Chama Cha Mapinduzi.“ameandika Mwigulu Nchemba kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Profesa Maji Marefu ameaga dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Soma zaidi taarifa ya kifo chake HAPA. 

Godbless Lema Aguswa Na Hali za Vigogo wa Escrow Wanaosota Mahabusu

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekiri kuwaone huruma watuhumiwa wa makosa ya uhujumu uchumi, wafanyabiashara Harbinder Seth pamoja na James Rugemalila kwa kuitaka serikali ikamilishe upelelezi kwani watu hao wanapitia mateso kwa kukaa mahabusu.
Lema ameonyesha kuguswa na watu hao baada ya picha zao kusambaa siku ya Jumatano hii walipokuwa wamekwenda kusikiliza kesi yao huku upande wa mashtaka wakidai kuwa bado upelelezi haujakamilika.
“Ninaona huruma juu yenu. Serikali kamilisheni upelelezi juu ya watu hawa kama wanastahili adhabu walipe walichopanda, kuwa mahabusu bila kesi yako kusikilizwa ni mateso kuliko mnavyoweza kufikiri”.
Ameongeza Pengine wanastahili adhabu lakini ni vyema Mahakama ifanye maamuzi.
Seth na Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu, kughushi na kutoa nyaraka za kughushi.

Pia, wanadaiwa kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola 22 milioni za Marekani na Sh309.46 bilioni

Neema kwa Vijana: Tazama Hapa Tangazo la Nafasi za Kazi Toka Jeshi la Polisi

TANGAZO LA AJIRA.


Jeshi la Polisi Tanzania linatangaza nafasi za ajira kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kwa vijana wa JKT wa Operesheni Kikwete waliopo nje ya kambi za JKT (waliomaliza mkataba wenye elimu ya kidato cha nne, sita, stashahada, stashahada ya juu na shahada.

Waombaji watatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

1.Awe nje ya kambi ya JKT. 
2. Awe Mtanzania kwa kuzaliwa. 
3. Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 25 kwa wenye elimu ya kidato cha nne, sita na stashahada.
4.Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi 28 kwa wenye elimu ya Stashahada ya juu na Shahada. 
5. Awe na elimu ya kidato cha nne aliyemaliza mwaka 2014, 2015 na 2016 mwenye ufaulu ufuatao:-
  • . Aliyemaliza mwaka 2014 awe na ufaulu wa GPA usiopungua 0.6
  •   Aliyemaliza mwaka 2015 na 2016 awe na ufaulu usiozidi alama (Points) 30.
6. Awe na elimu ya kidato cha sita aliyemaliza mwaka 2014, 2015 na 2016 na kufaulu. 
7. Awe na Stashahada aliyehitimu mwaka 2014, 2015 na 2016. 
8. Awe na Shahada aliyehitimu mwaka 2014, 2015 na 2016. 9. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa, vyeti vya taaluma (Academic Certificates) pamoja na vyeti vya kuhitimu elimu aliyonayo (Leaving Certificate/Transcript). 
10. Awe na picha 3 za rangi (passport size). 
11. Asiwe na kumbukumbu za uhalifu. 
12. Awe na afya njema (kimwili na kiakili) iliyothibitishwa na daktari wa serikali. 
13. Awe hajaoa/hajaolewa au kuwa na mtoto. 
14. Asiwe na alama za kuchora mwilini (Tattoo). 
15. Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania. 
16. Awe na urefu usiopungua futi tano inchi tano (5.5″) kwa wanaume na futi tano na inchi tatu (5.3) kwa wanawake. 
17. Waombaji watakaofaulu usaili ndio watakaochaguliwa. 18. Awe hajawahi kutumia madawa ya kulevya.
19. Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya Polisi. 
20. Awe hajaajiriwa na Taasisi nyingine. 
21. Waombaji wote waandike barua za maombi wao wenyewe kwa mkono (hand written) wakiambatanisha nakala za vivuli vya vyeti kwa anuani ifuatayo:- 
Inspekta Jenerali wa Polisi, 
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P 9141
 Dar es Salaam.

NB: Barua za maombi ziwasilishwe kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa ambapo mwombaji yupo. 
22. Waombaji wenye masomo/taaluma za Sayansi na Ufundi watapewa kipaumbele. 
23. Usaili utafanyika kwenye Ofisi ya Kamanda wa Mkoa husika. 
24. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 01/07/2018.

Kwa maelezo/ufafanuzi zaidi kuhusu nafasi, sifa na vigezo pamoja na tarehe ya kuanza usaili tembelea tovuti ya Polisi kwa anuani ifuatayo www.policeforce.go.tz au fika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa uliopo.

Swing Asli

IMUSSA A. TAIBU – ACP] 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Mzee Majuto Awasili Kutokea India, Afikishwa Muhimbili

Muigizaji nguli nchini Tanzania, Amri Athuman maarufu kama Mzee Majuto amewasili nchini na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Ny.0erere jijini Dar es Salaam akitokea nchini India alikokuwa amekwenda kwa ajili ya matibabu.

Mzee Majuto amewasili Airport leo Juni 22, 2018 majira saa 10 jioni na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo atakua hapo kwa muda ili kukutana na wataalam kwa ajili ya uangalizi kukamilisha matibabu yake.

Rais Magufuli Afanya Uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Yohana Luhunga Budeba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tanzania Agricultural Research Institute – TARI).


Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Budeba umeanza June 20, 2018.

Mitihani ya kidato cha sita yasababisha Intaneti kuzimwa


Serikali nchini Algeria imelazimika kuzima huduma ya Internet nchi nzima kuepuka udanganyifu katika mitihani ya kidato cha sita inayoendelea nchini humo. 

Imeelezwa kuwa pia vifaa vyote ambavyo hutumika kupatia huduma ya Internet vimekatazwa kufikishwa katika maeneo ya karibu ambapo mitihani hiyo inafanyika huku mitambo maalumu ikifungwa kubaini uwepo wa vifaa hivyo. 

Kwa mujibu wa Serikali huduma hiyo ya Internet itaendelea kukosekana kutokea June 21 mpaka June 25 siku ambayo mitihani itakuwa inamalizika. 

Aidha duru za kuaminika zinasema kuwa Serikali hiyo imeamua kuchukua uamuzi huo baada ya mitihani ya mwaka 2016 kuvuja sana kwenye mitandao ya kijamii hivyo wameamua kuzima Internet ili kubana upenyo wa mitihani hiyo kuvuja mitandaoni mwaka huu.

Inasikitisha! Ambaka Mama Yake Mzazi Kisha Kumchinja na Panga Hadi Kufa

Inasikitisha! Ambaka Mama Yake Mzazi Kisha Kumchinja na Panga Hadi Kufa
Mkazi wa mtaa wa Wang'waray mjini Babati mkoani Manyara anashikiliwa na polisi akidaiwa kumbaka mama yake mzazi, kisha kumuua kwa kumchinja akitumia panga.



Inadaiwa kuwa mkazi huyo ambaye anaishi nyumba moja na mama yake alifanya tukio hilo akiwa amelewa baada ya kuvuta bangi na kurudi nyumbani ambapo alimkuta mama yake pia amelewa pombe za kienyeji.



Akizungumza  leo Juni 21 na Mwananchi, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Asia Ramadhani alisema mwanamke huyo alifariki dunia Juni  19 saa 4 usiku akiwa nyumbani kwake katika mtaa huo.



Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Agustino Senga amesema mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 51, alifariki dunia kwa kukatwa shingoni na kitu chenye ncha kali baada ya kubakwa.



"Mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi kabla ya kufanyika kwa mazishi," amesema Kamanda Senga. 

Mbunge CCM Aibua Upya Sakata la Ununuzi wa Bombardier

Mbunge CCM Aibua Upya Sakata la Ununuzi wa Bombardier
Mbunge wa Ulyankulu (CCM), John Kadutu amesema ununuzi wa ndege za Bombardier uliofanywa na Serikali hauna tija kwa wananchi wa jimbo lake iwapo huduma za afya na barabara hazijaboreshwa.

Kadutu ametoa kauli hiyo leo Jumatano Juni 20, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Serikali mwaka 2018/19 bungeni mjini Dodoma.

Amesema umebaki mwaka mmoja kabla ya nchi kuingia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, hivyo ahadi zilizotolewa zinapaswa kutekelezwa.

“Serikali imejenga reli, inanunua ndege hebu twendeni kwa wananchi, ujue ukienda kule Ulyankulu ukauliza Bombardier hawakuelwi, barabara mbovu, afya mbovu hawakuelewi,” amesema Kadutu.

“Pelekeni fedha barabara ziboreshwe, Tarura (Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini) wapewe fedha. Bajeti iliyobaki ni moja ya kujadili kwa utulivu kwani akili itakuwa majimboni tu, tusaidieni ili mwaka 2020 tupete,” amesema.

Akigusia  ahadi za kampeni za uchaguzi, Kadutu amesema waliahidiwa jimbo la Ulyankulu litakuwa wilaya lakini mpaka sasa ahadi hiyo haijatekelezwa.

“Hamtaki kutupa eneo lakini mnasema ahadi za Rais zitatekelezwa, sasa hii ni ahadi ya Rais, alisema akiingia siku tatu tu tunapata wilaya,” amesema.

“Sasa imebaki mwaka mmoja tu na nusu yako mengi, mmetuahidi lami tena kilomita tatu tu lakini tunaona mambo ambayo hayako katika ilani yanatekelezwa. Tukisema…,mimi watu wa Ulyankulu wamenituma.”

Mbunge huyo amesema anashangazwa na mawaziri kutotembelea jimboni kwake huku wakionekana kupishana katika majimbo mengine jambo linalokatisha tamaa wananchi.