Breaking News: Wema Sepetu ahukumiwa jela mwaka mmoja kwa Madawa ya Kulevya

Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya milioni 2 baada ya kukutwa na makosa mawili ya kutumia na kuhifadhi dawa za kulevya aina ya Bangi nyumbani kwake.

Akisomewa hukumu hiyo leo Julai 20, 2018 katika Makahama ya Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam, Wema Sepetu ametakiwa kulipa faini hiyo na kama akishindwa basi atapelekwa jela kutumikia adhabu hiyo.

Katika hukumu nyingine wafanyakazi wawili wa ndani wa msanii huyo ambao nao walitajwa kwenye kesi hiyo wameachiwa huru na mahakama hiyo kwa kukutwa bila hatia.
==

No comments:

Post a Comment

paulmkale