Neema kwa Vijana: Tazama Hapa Tangazo la Nafasi za Kazi Toka Jeshi la Polisi

TANGAZO LA AJIRA.


Jeshi la Polisi Tanzania linatangaza nafasi za ajira kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kwa vijana wa JKT wa Operesheni Kikwete waliopo nje ya kambi za JKT (waliomaliza mkataba wenye elimu ya kidato cha nne, sita, stashahada, stashahada ya juu na shahada.

Waombaji watatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

1.Awe nje ya kambi ya JKT. 
2. Awe Mtanzania kwa kuzaliwa. 
3. Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 25 kwa wenye elimu ya kidato cha nne, sita na stashahada.
4.Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi 28 kwa wenye elimu ya Stashahada ya juu na Shahada. 
5. Awe na elimu ya kidato cha nne aliyemaliza mwaka 2014, 2015 na 2016 mwenye ufaulu ufuatao:-
  • . Aliyemaliza mwaka 2014 awe na ufaulu wa GPA usiopungua 0.6
  •   Aliyemaliza mwaka 2015 na 2016 awe na ufaulu usiozidi alama (Points) 30.
6. Awe na elimu ya kidato cha sita aliyemaliza mwaka 2014, 2015 na 2016 na kufaulu. 
7. Awe na Stashahada aliyehitimu mwaka 2014, 2015 na 2016. 
8. Awe na Shahada aliyehitimu mwaka 2014, 2015 na 2016. 9. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa, vyeti vya taaluma (Academic Certificates) pamoja na vyeti vya kuhitimu elimu aliyonayo (Leaving Certificate/Transcript). 
10. Awe na picha 3 za rangi (passport size). 
11. Asiwe na kumbukumbu za uhalifu. 
12. Awe na afya njema (kimwili na kiakili) iliyothibitishwa na daktari wa serikali. 
13. Awe hajaoa/hajaolewa au kuwa na mtoto. 
14. Asiwe na alama za kuchora mwilini (Tattoo). 
15. Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania. 
16. Awe na urefu usiopungua futi tano inchi tano (5.5″) kwa wanaume na futi tano na inchi tatu (5.3) kwa wanawake. 
17. Waombaji watakaofaulu usaili ndio watakaochaguliwa. 18. Awe hajawahi kutumia madawa ya kulevya.
19. Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya Polisi. 
20. Awe hajaajiriwa na Taasisi nyingine. 
21. Waombaji wote waandike barua za maombi wao wenyewe kwa mkono (hand written) wakiambatanisha nakala za vivuli vya vyeti kwa anuani ifuatayo:- 
Inspekta Jenerali wa Polisi, 
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P 9141
 Dar es Salaam.

NB: Barua za maombi ziwasilishwe kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa ambapo mwombaji yupo. 
22. Waombaji wenye masomo/taaluma za Sayansi na Ufundi watapewa kipaumbele. 
23. Usaili utafanyika kwenye Ofisi ya Kamanda wa Mkoa husika. 
24. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 01/07/2018.

Kwa maelezo/ufafanuzi zaidi kuhusu nafasi, sifa na vigezo pamoja na tarehe ya kuanza usaili tembelea tovuti ya Polisi kwa anuani ifuatayo www.policeforce.go.tz au fika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa uliopo.

Swing Asli

IMUSSA A. TAIBU – ACP] 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment

paulmkale