MSHAMB-ULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Amissi Tambwe raia wa Burundi ameibuka na kuweka wazi kwamba katika kipindi hiki cha usajili hana mpango wowote wa kuondoka ndani ya timu hiyo kutokana na kujiona ana deni la kulilipa baada ya kushindwa kuonyesha makali msimu uliopita.Mshambuliaji huyo hakuwa na msimu mzuri katika msimu uliomalizika hivi karibuni baada ya kuandamwa na majeraha ya kila mara ya goti ambayo yalimsababisha kumaliza ligi akiwa hajafunga bao lolote lile.
Akizungumzia juu ya mustakabali wake
ndani ya kikosi hicho, Tambwe ambaye yupo kwao kwa ajili ya mapumziko
baada ya ligi kumalizika mshambuliaji huyo amesema hawezi kuondoka
katika timu hiyo kwa sasa kufuatia kuvumiliwa kwa msimu mzima huku akiwa
na majeraha ya mara kwa mara ambapo anataka kulipa fadhila kwenye msimu
ujao.
“Kwa msimu uliopita sikuwa na kiwango
kikubwa hivyo ninajiona kwamba nina deni la kulipa kwa Yanga ambao
wamenivumilia licha ya kwamba nilikuwa na majeraha, ninachofanya sasa ni
kujiandaa kwa ajili ya msimu ujao niwe vizuri,” alisema mshambuliaji
huyo.
No comments:
Post a Comment
paulmkale