Ujumbe wa mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye katika akaunti yake ya Twitter, umeibua mjadala kuanzia jana hadi leo.
Katika mjadala Nape hakuwa nyuma katika kujibizana na wafuasi wake wanaomuunga mkono huku wengine wakimkosoa.
Jana Nape alituma ujumbe ulioambatana na picha ya simba, kisha akaandika,‘Watashindana lakini hawatashinda’.
Katika picha hiyo, pia aliambatanisha kifungu cha Biblia kutoka Daniel 6:16 kinachosema: “Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Daniel, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena akamwambia Daniel, Mungu wako unayemtumikia, daima yeye atakuponya.”
Dakika chache tu baada ya kutuma ujumbe huo, wafuasi wake walianza kumponda huku wengine wakimuunga mkono.
No comments:
Post a Comment
paulmkale