Baada ya Kutumbuliwa Mwigulu Aongea Haya Kuhusiana na Kifo cha Maji Marefu

Baada ya Kutumbuliwa Mwigulu Aongea Haya Kuhusiana na Kifo cha Maji Marefu
Kufuatia kifo cha Mbunge wa Korogwe vijijini (CCM), Stephen Ngonyani almaarufu kama Profesa Maji Marefu kilichotokea usiku wa jana, kimemuibua aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Mwigulu ambaye amevuliwa uwaziri na Rais Magufuli wikiendi iliyopita amesema kuwa CCM imepata pigo kwa kumpoteza kada na kiongozi wa kweli.

“Maandiko matakatifu yanasema, Mwanadamu aliyezaliwa na Mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, Tumempoteza kaka,ndugu na rafiki Comrade Stephen Hilary Ngonyani (Prof.MajiMarefu), tumempoteza Kiongozi na kada kweli kweli wa Chama Cha Mapinduzi.“ameandika Mwigulu Nchemba kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Profesa Maji Marefu ameaga dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Soma zaidi taarifa ya kifo chake HAPA. 

No comments:

Post a Comment

paulmkale