Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekiri kuwaone huruma watuhumiwa wa
makosa ya uhujumu uchumi, wafanyabiashara Harbinder Seth pamoja na
James Rugemalila kwa kuitaka serikali ikamilishe upelelezi kwani watu
hao wanapitia mateso kwa kukaa mahabusu.
Lema
ameonyesha kuguswa na watu hao baada ya picha zao kusambaa siku ya
Jumatano hii walipokuwa wamekwenda kusikiliza kesi yao huku upande wa
mashtaka wakidai kuwa bado upelelezi haujakamilika.
“Ninaona
huruma juu yenu. Serikali kamilisheni upelelezi juu ya watu hawa kama
wanastahili adhabu walipe walichopanda, kuwa mahabusu bila kesi yako
kusikilizwa ni mateso kuliko mnavyoweza kufikiri”.
Ameongeza Pengine wanastahili adhabu lakini ni vyema Mahakama ifanye maamuzi.
Seth
na Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kula
njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu, kughushi na kutoa nyaraka za
kughushi.
Pia,
wanadaiwa kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na
kusababisha hasara ya Dola 22 milioni za Marekani na Sh309.46 bilioni
No comments:
Post a Comment
paulmkale