DIAMOND PLATINUMZ AMCHEFUA WEMA! bofya hapa kupata tarifa kamili

KAULI ya nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz ’ kwamba hawezi kuoa
kamwe, inadaiwa kumchefua mwandani wake ,
Wema Isaac Sepetu ‘ Beautiful Onyinye’,
Aliporejea Bongo kutoka Marekani juzikati ,
Diamond alitoa kauli hiyo na kuandikwa
kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti la
Ijumaa, toleo la wiki iliyopita likiwa na
kichwa cha habari; ‘DIAMOND : SITAOA
KAMWE’ ambapo ndani yake alieleza jinsi
ambavyo mastaa wengi waliooa wameanguka
kisanii.
MTU WA KARIBU AYASEMA YA WEMA
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa hao ,
Wema hakufurahishwa na habari hiyo kwa
sababu anajua yeye ndiye mke mtarajiwa wa
Diamond.
Ilidaiwa kwamba, Wema alijikuta akipoteza ile
furaha ya kwamba wawili hao wangefunga
ndoa mwezi huu (Agosti) kama ilivyotabiriwa
na mnajimu maarufu Bongo, Maalim Hassan
Yahya Hussein.
“Baada ya kauli hiyo ya Diamond na kutotimia
kwa utabiri wa Maalim Hassan kwa sababu
hakuna hata dalili za maandalizi ya tukio hilo
muhimu kwenye maisha ya mwanadamu ,
Wema ameanza kukata tamaa , lakini amesema
hawezi kulazimisha ndoa kwa mwanaume kwa
kuwa si utamaduni wa wanawake wa
Kitanzania wala Kiafrika.
“Unajua Kibongobongo au hata Kiafrika hai -
sound vizuri na pengine haiwezekani kwa
mwanamke kulazimisha kuolewa kama
mwanaume hataki. Hicho ndicho kilichomtibua
Madam (Wema ) baada ya kusoma
alichokisema Diamond ,” kilisema chanzo hicho
na kuongeza:
“Wema amehisi yeye ni girl lover ( mpenzi ) tu
kwa Diamond na si wife material (mke mwema)
kwa hiyo anawaza sana kuhusiana na ishu
hiyo japo mahaba niue kati yao yanaendelea ,
lakini anafikiria kuchukua uamuzi mzito . ”
WEMA SASA
Mwanadada huyo alisema kuwa kwa sasa
haumizi tena kichwa kuhusu suala la ndoa na
Diamond na kwamba hana haraka nalo.
“Mimi naamini sana mambo ya utabiri, lakini
siumizi kichwa na suala la kuolewa na
Diamond na kamwe siwezi kumlazimisha
anioe.
“Kikubwa katika mapenzi ni upendo wa kweli
ambao ananionesha bila kipimo. Wala sina
papara, hata kama mtabiri kasema ndoa yetu
ni lazima ifungwe mwaka unaogawanyika kwa
mbili kwa maana ya mwaka 2016 kama
itashindikana mwezi huu , hilo kwangu si tatizo
la kunifanya nililie kuolewa na Chibu (Diamond ).
“Ninachojua mimi Mungu ndiye anapanga yote
na kama ndoa ipo ipo tu maana kuna watu
wapo kwenye ndoa na hawana upendo wa
kweli kama tulionano sisi ,” alisema Wema .
MAMA WEMA ANASEMAJE ?
Paparazi wetu alimtwangia simu mama yake
Wema, Mariam Sepetu na kumuuliza mambo
mawili, kuhusu bintiye kuvishwa pete ya ndoa
na Diamond na suala la Mbongo Fleva huyo
kusema hataoa kamwe !
“Mimi niseme nini ? Sina la kusema kuhusu
Wema. Mambo yake ni yake mwenyewe na
huyo Diamond wake . Kwanza kwa nini mnipigie
mimi, si mumtafute yeye mwenyewe?” alisema
mama huyo kwa sauti ya utulivu .
MAMA DIAMOND AFUATA NYAYO
Katika hali ya kushangaza, mama Diamond,
Sanura Kasim ‘ Sandra’ ameonekana kunawa
mikono kwa kauli aliyowahi kuitoa siku za
nyuma kuhusu mtoto wake na masuala ya
kutooa au kuoa .
Nasibu ni mtu mzima sasa , siwezi kumpangia
lolote kuhusu kuoa au kutooa . Wakati ukifika,
anaweza kusema lolote ambalo ataliona ni zuri
katika maisha yake .”
KUHUSU PETE YA NDOA
Kuhusu Diamond kumvisha pete ya ndoa
Wema, tendo ambalo lilifanyika hivi karibuni
wakiwa nchini Afrika Kusini, Amani lilifanikiwa
kuzungumza na shehe mmoja ambaye aliomba
hifadhi ya jina lake ambapo alisema
alichokifanya Diamond kwa Wema ni usanii.
“Diamond amemfanyia usanii mwenzake . Pete
gani bila kufunga ndoa. Halafu katika Uislam ,
hakuna tendo la wanandoa kuvalishana pete,
hayo mambo wanayafanya wenyewe, ” alisema
shehe huyo .
WEMA AIZUNGUMZIA PETE
Wema alipopewa nafasi ya kuizungumzia pete
hiyo alisema Diamond aliipenda tu akaamua
kumnunulia na kumvisha lakini haihusiani na
ndoa.
“Sisi ( na Diamond ) tulikuwa Afrika Kusini, baby
wangu akaipenda pete, akainunua na
kunivalisha , haina uhusiano na ndoa ,” alisema
Wema.

No comments:

Post a Comment

paulmkale