Ommy Dimpoz |
“Katika nyimbo zangu nilizowahi kutoa naweza kusema watu walishazoea wimbo wiki moja tu tayari wimbo umeshahit. Lakini nyimbo ikiwa namna hiyo inachangia kutokaa muda mwingi. Lakini ukiangalia Ndagushima imeanza taratibu sana ni kama nyimbo ambayo inakuwa inasearch,” amesema Ommy.
“Nimegundua ni nyimbo kubwa sana katika tour zangu ambazo nazunguka. Hata watu nikiwauliza ‘nyimbo gani mnataka’ wanasema Ndagushima. Hata nikipita mtaani watu wananiita ‘Mr Ndagushima’. Watu wanashindwa kuelewa nyimbo isipofanya vizuri sio sababu ya msanii kwamba ndo labda ameshachemka au nguvu imepungua, hapana. Hii ipo duniani kote kwa wasanii wote sio hapa tu sio kwangu mimi hata kwa wasanii wa hapa Tanzania.”
“Wasanii wote unaowajua wewe sometimes wanaweza wakatoa nyimbo na inaweza ikafall, sio mimi tu hata akina Jay Z, akina Rihanna wanatoaga nyimbo na hazifanyi vizuri. Lakini sisemi kuwa Ndagushima haijafanya vizuri ni nyimbo ambayo ilikuwa inahitaji muda nafikiri watu wanaona. Kuna wengine walikuwa wananishauri kwamba toa nyimbo nyingine, kwasababu wamesikia nyimbo zangu ambazo ziko studio mimi nikasema no kadri muda unavyokwenda nitatoa nyimbo nyingine,” ameongeza.
Katika hatua nyingine, Ommy amezungumzia ujio wake mpya ambao amedai ni kolabo ya msanii wa kimataifa.
“Sio kwamba Ndagushima ndo tumefunga mwaka, kuna ujio wa surprise ya video nyingine na hot kolabo. Kwahiyo watu watarajie hilo, ni msanii mkubwa wa nje, kwa sasa hivi hatuwezi kumsema.”
No comments:
Post a Comment
paulmkale