Random Thoughts: Ni filamu nyingi mpya za Bongo zinaingia sokoni kila siku, lakini kwanini hamzifanyii promo?

Kiwanda cha filamu za Tanzania maarufu kama Bongo Movies kiko busy kuliko unavyoweza kudhani. Kiko busy kuliko hata enzi za uhai wa Steven Kanumba ambaye wengi tunamchukulia kama mtu muhimu aliyezipa ‘hadhi ya kueleweka’ filamu hizo.Utagundua kiwanda hicho kilivyo busy kama ukitembelea maduka ya kuuza filamu ukiona posters kibao zilizobandikwa kwenye mitaa mbalimbali katika mikoa mingi ya Tanzania. Utakutana na movie nyingi mpya zilizotoka na ambazo hujawahi kuzisikia zikizungumzwa sehemu yoyote ile.

Kila siku, filamu nyingi mpya za Tanzania zinaingia sokoni na asilimia 70, zinaingia kimya kimya. Kidogo kwa wale waigizaji wanaotumia vizuri Instagram na mitandao mingine ya kijamii, utaona wamekuwa wakipost picha za makava ya filamu hizo na hivyo kukuza uelewa wa uwepo ama ujio wa kazi zao mpya.

Vipi kwa Watanzania wasiotumia mitandao ya kijamii? Hawa watajuaje kuwa kuna filamu mpya imeingia? Sawa, zipo posters. Lakini unadhani poster pekee inaweza kuwa na ushawishi? Sidhani.Kwa leo nisingependa kuzungumzia udhaifu uliopo kwenye filamu zetu, ambao kiukweli ni mkubwa lakini nitajikita katika kuangaza kasoro ya kutokuwepo kwa promotion katika filamu zinazotoka.

Waigizaji, watayarishaji na makampuni machache ya usambazaji yaliyopo, hawaoneshi jitihada zinazostahili katika kufanyia promotion kazi zao zinazoingia sokoni.

Haitoshi kuishia kupost cover la filamu kwenye Instagram au Facebook. Haitoshi kutengeneza posters na kuzibandika mtaani. Filamu mpya zinahitaji promo ya nguvu. Utamshawishi vipi mpenzi wa filamu za Tanzania kama humtamanishi kwa promo nzuri ya filamu yenyewe?

Kuna njia mbalimbali za kupromote filamu ambazo ni pamoja na press release, kampeni za matangazo, kufanya mahojiano na watu muhimu kwenye filamu kama waigizaji au waongozaji nk. Hizi ni njia tatu muhimu na zinazowekana kufanyika katika kufanya promotion ya filamu.

Trailers

Asilimia kubwa ya filamu za Tanzania huingia sokoni bila kuwa na trailer. Na hata zile zenye trailer, trailer hizo mara nyingi utaziona mwanzoni mwa filamu mpya utakayonunua. Mtu kama mimi ambaye sinunui tu filamu hivi hivi, nitaiona vipi trailer hiyo? Kwa kawaida trailer za filamu hutoka miezi kadhaa kabla ya filamu kutoka na sehemu pekee trailer huangaliwa ni mtandaoni hususan kwenye Youtube. Trailer nzuri inaweza kuwa na ushawishi mkubwa kwa wapenzi wa filamu.

 Matangazo ya TV na Radio

Baadhi ya waigizaji wanaweza kujitetea kuwa bajeti haitoshi lakini mimi napingana na hilo. Uwezo wa kulipa matangazo ya redio au TV wanao lakini kwakuwa hawafahamu umuhimu wake, hili hulizembea. Gharama za matangazo kwenye redio na TV hazitishi kiasi hicho. Mbona watu wana maduka ya nguo au biashara za kawaida tu wanaweza kumudu? Ni lini mara yako ya mwisho umeona tangazo la movie mpya ya Kibongo kwenye TV? Ni lini umesikia tangazo zuri la filamu ya Kibongo kwenye redio?

Kwa taarifa yako, wasambazaji wa filamu wa Hollywood hutumia takriban dola bilioni 4 za Kimarekani kulipia matangazo ya TV yenye sekunde 30 ama kuweka matangazo kwenye magazeti.

 Promotional tours na interviews

Mfano mzuri wa point hii ni kile anachokifanya Alikiba kwa sasa ambapo amekuwa akitembea kwenye vyombo karibu vyote vya habari kufanya interview ili kupromote kazi zake mpya ‘Mwana’ na Kimasomaso’. Waigizaji wa filamu wanaweza pia kufanya hivi, inawezekana sana.

Utafiti unaonesha kuwa baada ya Nigeria, Tanzania ndio inafuata kwa kuwa na kiwanda cha filamu kinachofanya vizuri kibiashara. Waigizaji na wasambazaji wa filamu wanatakiwa kuwa aggressive zaidi katika kuzifanyia promo kazi zao.


No comments:

Post a Comment

paulmkale