Banana Zorro amshirikisha Young Killer kwenye single mpya ‘Samehe Sahau’, aanza kushoot video na AJ

Banana Zorro leo ameanza kushoot video ya single yake mpya anayotarajia kuiachia wiki mbili zijazo, inayotayarishwa na mwongozaji Adam Juma wa Next Level.Dully Sykes ndio ame produce hiyo nyimbo, Dully akaniambia itakuwa poa kama ukifanya na new blood kama Young Killer nini itakuwa vizuri zaidi, nikamcontact Young Killer…actually he is a good rapper na ana styles flani ambazo zina
match na style zangu kwa namna moja ama nyingine, kwa mfano hata hii nyimbo tunayofanya ni Rock, R&B, Bongo Fleva”. Alisema Banana

Ni zaidi ya mwezi mmoja umepita toka rapper huyo wa Mwanza aachie single yake ‘Umebadilika’ aliyomshirikisha Banana.

Banana pia amezungumzia alichokuwa anafanya kipindi chote alichokaa kimya:

“Kitu ambacho watu wengi hawafahamu ni kwamba, unajua muda mwingi ambao nilikuwa nimekaa kimya nilikuwa niko kimya kwa sababu nilikuwa najaribu kuangalia na kujiuliza wapi nilipokosea, na kitu gani kinachotakiwa kibadilishwe ili tuweze kusonga mbele…kwasababu asilimia kubwa ya wasanii wengi wa kibongo ambao mimi nimeanza nao zamani badala ya kukaa na kufikiria jinsi gani ya kujikwamua au kwenda mbele mtu anafikiria tu lazima mtu flani atokee aje kunisaidia…unajua mi nina biashara nyingine ya live band ambayo inani tight lakini sasa hivi tuko sawa, nimeweza kubalance muda.”

No comments:

Post a Comment

paulmkale