Ben Pol kusheherekea birthday yake Jumatatu (Sept 8) na watoto wenye maradhi mbalimbali walioko Muhimbili

Jumatatu ya Tarehe 8 septemba ni siku ya kuzaliwa mwimbaji wa R&B Tanzania, Ben Pol. Na katika kusheherekea siku hiyo mwimbaji huyo wa ‘Jikubali’kuwa atajumuika na watoto wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali walioko katika
hospitali ya Muhimbili kitengo cha MOI, ili kuwapatia misa“Nimefikiria kutembelea kitengo cha watoto hasa watoto wenye matatizo ya uvimbe wa kichwa wale ambao wako MOI, nimeamua mimi pamoja na ndugu na marafiki na watu wote ambao watapenda kujumuika waungane na mimi pia hiyo Jumatatu tarehe 8 mwezi wa tisa saa sita mchana pale MOI. Mimi nitakuwepo nitakuwa napokea marafiki, wageni mashabiki ambao watapenda kujumuika pamoja na wenyeji wetu pale walezi wauguzi pale watatukaribisha, tutajumuika nao tutatoa zawadi ambazo tutakuwa tumejaaliwa siku hiyo then jioni ndo tunaweza kuzungumza mambo kama ni party na nini.” Amesema Ben Pol.

Kupitia Instagram pia amepost:

No comments:

Post a Comment

paulmkale