Kwa Mara Nyingine tena Diamond Platinumz(@diamondplatinumz) kuchuana na Davido kwenye tuzo za MTVEMA

Majina ya wasanii wa Afrika watakaowania tuzo za MTV Europe, MTVEMA yametangazwa na Diamond ni miongoni mwa wasanii watakaowania tuzo hizo zitakazotolewa November 9 jijini Glasgow, Scotland.Diamond atachuana na
Davido, Toofan wa Togo na Goldfish wa Afrika Kusini.Hata hivyo mashabiki mwaka huu wamepewa fursa ya kumtaja msanii mwingine wa tano atakayewania tuzo hiyo. Wasanii sita wanaowania nafasi iliyosalia ni:

Anselmo Ralph – #NominateAnselmoRalph
 Gangs of Ballet – #NominateGangsOfBallet
 Mafikizolo – #NominateMafikizolo
 Sarkodie – #NominateSarkodie
 Sauti Sol – #NominateSautiSol
 Tiwa Savage – #NominateTiwaSavage

Kura za wild card kupitia Twitter zitafanyika hadi September 14 na majina yote ya “2014 MTV EMA” yatatangazwa September 16 na upigaji kura kuanza rasmi.

Soma zaidi kuhusu tuzo hizo hapa

Katika hatua nyingine msanii huyo ameshinda tuzo ziitwazo Afro Australia Music & Movie Awards AAMMA2014 kwa wimbo alioshirikishwa na Dezert Eagle ‘Everyday kama wimbo bora wa kushirikiana.

No comments:

Post a Comment

paulmkale