Polisi Ujerumani wamnusuru Diamond kutoka kwa mashabiki wenye hasira baada ya kuingia ukumbini saa 10 alfajiri(NISHEEDAH)

Kama isingekuwa polisi wa Ujerumani leo tungekuwa tunaongea habari nyingine kwakuwa Diamond Platnumz aliponea chupuchupu kushambuliwa na mashabiki wenye hasira jijini Stuttgart nchini humo baada ya kuingia ukumbini saa 10 Alfajiri wakati mashabiki hao walikuwa wakimsubiri tangaa saa 4 usiku.Inaendelea..........

Uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye ukumbi ambao Diamond alikuwa anatarajia kutumbuiza jijini Stuttgart

Show hiyo ilikuwa ifanyike usiku wa kuamkia jana.

Katika tukio hilo lililoandikwa na vyombo vya habari vya nchini Ujerumani, promota wa show hiyo ambaye ni Mnaijeria alikimbia eneo la tukio na DJ wa show kupewa kipondo cha paka mwizi.

Story kutoka Ujerumani inasema:

 Majira ya saa 10 alfajiri Mwanamuziki nyota wa Bongo Flava Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijukuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na polisi mjini Stuttgart,Ujerumani,baada ya mashabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show. Mashabiki hao waliokuwa wamelipa tiketi kwa Euro 25 kama kiingilio waliahidiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijikuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 alfajiri ndipo Diamond alipopelekwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.

Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake. Kilichowakera zaid mashabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki ma-Djs walishambuliwa na wapo Hospitalini kwa sasa

No comments:

Post a Comment

paulmkale