zasababisha hasara ya euro 300,000 Stuttgart, Ujerumani - Anayejiita promota Biritts
jumla ya hasara ya Euro 300,000 (Tsh.600 million)
zilizo sababishwa na fujo ya siku ya Jumamosi 30
Agosti 2014 baada ya msanii wa Nasib Abdul aka
Diamond Platnumz kuchelewa kufika ukumbini
mjini Stuttgart, Ujerumani.
Baada ya uchunguzi wa polisi kufuatia fujo hizo
imegundulika kuwa muandaaji wa onyesho hilo Mr.
Awin Williams Akpomiemie aliudanganya utawala
wa ukumbi wa Sindfingen kwa kukodisha
ukumbi huo kwa ajili ya African Party na mkutano,
sio onesho la muziki kama alivyofanya na
kusababisha fujo zilizotia hasara ya euro 300,000
(shilingi millioni 600=) ambazo inatakiwa alipe.
Promota huyo Awin Williams Akpomiemie hakuwa
na bima ya ku-cover au kulinda onyesho hilo na
ukumbi lilipofanyika ambapo ni ukumbi wa
mikutano na maonesho ya bidhaa na siyo muziki.
Taarifa za uhakika zinasema kuwa polisi
imelipeleka suala hilo kwa ofisi ya sheria (Stadt
Anwalt) ya mji wa Stuttgart ili ichukue mkondo wa
sheria. Polisi pia inaendelea kumuhoji kwa
kujihusika na biashara nyingine haramu.
Wakati huo huo, taasisi mbalimbali na jumuiya za
wafrika nchini Ujerumani na jirani zimelaani vikali
tabia za raia huyo wa nigeria Awin Williams
Akpomiemie za kuwadanganya washabiki na
kulivunjia adhi sifa za bara la Afrika nchini
Ujerumani. Taasisi na jumuiya hizo zimewaonya
watu kujiepusha kabisa na Mnaijeria huyo wa
Britts Events, Awin Williams Akpomiemie.
Magazeti mbalimbali nchini Ujarumani na nchi za
Afrika yameandika habari hii.
No comments:
Post a Comment
paulmkale