Serengeti Fiesta kufanyika mjini Musoma Jumapili hii

TAMASHA la Serengeti fiesta lililokuwa lifanyike jana Ijumaa katika Uwanja wa Karume mjini Musoma na kuahirishwa kutokana na ajali mbaya ya gari iliyotokea mjini humo sasa linatarajiwa kufanyika Jumapili ya
 leo jioni katika uwanja huo huo imeelezwa.Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Ephraim Mafuru alisema
kampuni yao pamoja na waandaaji wa tamasha hilo walichukua uamuzi wa kuahirisha ili kuwapa nafasi wakazi wa mji huo na kila aliyeguswa na tukio hilo kufuatilia kwa karibu taarifa zake.

“Kwa niaba ya timu nzima ya Kampuni ya Bia ya Serengeti, na uongozi wa SBL nina huzuni kubwa kutokana na tukio hili lililochukua uhai wa wapendwa wetu, tunatoa rambirambi zetu kwa ndugu wa marehemu wote na tunawatakia wajeruhi wapate nafuu mapema,” alisema.

Kutokana na tukio hilo wawakilishi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti pamoja na wasanii walioko Musoma katika ziara ya tamasha la Serengeti fiesta waliwatembelea majeruhi waliolazwa hospitalia na pia kutoa mkono wa pole kwa wafiwa.

Wasanii wanaotarajiwa kupanda jukwaani katika onyesho la jioni ya kesho ni pamoja na Stamina, Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Christian Bella, Chege, Mheshimiwa Temba, Young Killer, Shilole, Niki II, Recho na Barnaba huku wakisindikizwa na wasanii chipukizi wa maeneo mbalimbali ya Musoma na vitongoji vyake.

Tamasha hilo la Serengeti fiesta pia litaambatana na shughuli mbalimbali za buruda ni kama vile Serengeti Soka Bonanza na shindano la dansi la Serengeti fiesta, na kumtafuta Serengeti Super Nyota Diva’s.

No comments:

Post a Comment

paulmkale