Kaa Tayari;Ommy Dimpoz Kuachia Video Ya Tupogo Rimex

ommy
  1. Ommy Dimpoz ameamua kufanya remix ya hit song yake ‘Tupogo’ambayo alimshirikisha staa wa Nigeria J. Martins, wimbo ambao licha ya kufanya vizuri lakini uliacha deni la video ambayo ilishindikana kufanyika.

  2. Meneja wa Dimpoz ajulikanaye kama Mubenga amezitaja sababu za kuamua kufanya remix ya wimbo huo, pamoja na mipango ya kuifanyia video.


  3. “Sababu kubwa kwanza ya kufanya remix ya huu wimbo (Tupogo), ni wimbo ambao ulikuwa umependwa sana katika nyimbo zetu,”
    Mubenga aliiambia E-News ya EATV. “na katika nyimbo ambazo zimehit haraka basi Tupogo imehit haraka sana. Kwahiyo ni wimbo mkubwa ambao nafikiri ulipendwa kwa haraka, na kwa kuwa kila sehemu ambayo tulikua tukienda tulikua tukiulizwa video video video unajua ilikua inatuumiza sana, na mimi katika usimamizi wangu waga ndio napenda kukosolewa…kwasababu huwezi kujua kila kitu, lakini moja ya vitu vilivyokuwa vinaumiza nilivyokuwa naulizwa video ya Tupogo vipi. Kwahiyo this time around tumeamua kufanya remix kwaajili ya kuifanyia video moja kwa moja”.

No comments:

Post a Comment

paulmkale