Nuhu Mziwanda Achora Tattoo Nyingine Yenye Alama Shishi Baby

Nuh-Mziwanda-Na-Shilole

Wakati Nick Cannon ametoka kufunika Tattoo yenye jina la mke wake Mariah Carey ambaye wametengana kwa kuongeza mchoro mwingine juu yake hivi karibuni, msanii wa Bongo Fleva Nuh Mziwanda ameongeza Tattoo ya pili ya mpenzi wake Shilole kwenye mkono wake.

Nuh amesema mchoro huo wa pili kwenye mwili wake una sura ya Shishi baada ya ile ya kwanza ambayo ni jina la ‘Shishi Bybee’.

“Tattoo ya pili ni sura aisee sura ya mpenzi wangu Shishi,”
ameiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm. “nimetaka kuweka maana ya jina pamoja na sura yake unajua jina tu lilikuwepo kukamilisha upendo ule na thamani na shkurani kwake so nilichora ile Shishi Bybee ya maneno halafu baadae nimechora sura yake, nimechora mkono ule ule, so hii shishi Bybee iko nyuma ya mkono wangu halafu hii sura yake iko mbele.”

Nuh na Shishi

Mziwanda ameongeza kuwa mchoro huo umegharimu shilingi laki nne na nusu.

“Tattoo nimechora juzi, tumetumia kama laki nne hivi nne na nusu ukijumlisha na usafiri sababu jamaa alikua katoka Arusha. Ile ya mwanzo iligharimu kama laki mbili mbili na nusu”.

No comments:

Post a Comment

paulmkale