Bofya kupata Taarifa Kamili Kuhusu Mechi Hiyo
Wachezaji wa Mtibwa wakishangilia bao baada ya kuifunga Mbeya City |
Kikosi cha Mtibwa kilichoilambisha Mbeya City Bao 2-0 katika uwanja wa nyumbani |
Mchezaji wa Mbeya City Steven Mazanda akimdhibiti mshambuliaji wa Mtibwa Mussa Mgosi. |
Wachezaji wa Mtibwa wakishangilia bao la kwanza. |
Wachezaji wa Mbeya City wakitoka uwanjani baada ya kumalizika kwa mechi kati yao na Mtibwa, Mbeya City ililala 0-2 dhidi ya Mtibwa. |
Kikosi cha kutuliza ghasia FFU kilikaa tayari kwa ghasia zilizotaka kuibuka baada ya Mbeya City kufungwa bao la 2 na Mtibwa |
Kocha wa timu ya Mtibwa Meck Mexime akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo ulioopa ushindi timu yake. |
by paul mkale
TIMU ya Mtibwa ya mjini Morogoro leo
jioni imeifundisha kabumbu timu ya Mbeya City kwa kuilambisha jumla ya
magoli 2-0 katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.
Mbeya City ambayo imepoteza mechi ya
pili katika uwanja wa nyumbani baada ya wiki iliyopita kufungwa na Azam
1-0, ilishindwa kuutawala mpira katika dakika zote za mchezo.
Mpira ulianza kwa kasi huku kila timu
ikijitahidi kusaka bao lakini dakika ya 21 ya mchezo mpira wa kona
uliopigwa na David Luhende na kumkuta Amri Ally aliyeutingisha wavu wa
Mbeya City.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Mbeya City walikuwa nyuma kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kama ilivyokuwa
katika kipindhi cha kwanza timu zilishambuliana kwa zamu huku, Mtibwa
wakilihami goli lao na kutaka kuongeza bao nao Mbeya City wakijitahidi
kulishambulia lango la Mtibwa bila mafanikio.
Kila timu ilifanya mabadiliko katika
kipindi cha pili ambapo kwa upande wa Mtibwa Mussa Mgosi alitoka na
nafasi yake kuchukuliwa na Vicent Barnabas ilhali Mbeya City ilimtoa
Saad Kipanga na nafasi yake kuchukuliwa na Mwagane Yeya.
Mabadiliko hayo ya kila timu
yalibadilisha kidogo hali ya mchezo ambapo ari na nguvu mpya ya mpira
ilianza kuonekana kwa kila upande.
Hata hivyo ilikuwa ni dakika ya 78 ya
mchezo mchezaji wa Mtibwa aliyeingia kipindi cha pili Vicent Barnabas
aliwainua wapenzi wake kwa kuifungia Mtibwa bao la pili na kuzua
kizaazaa kwa upande wa mashabiki wa Mbeya City ambao walianza kuwarushia
mawe na chupa za maji wachezaji wa Mtibwa ambao walikuwa wakishangilia
bao hilo.
Hali hiyo ilisababisha kikosi cha
kutuliza ghasia kuwasha gari lake la washawasha na kutoa alama ya
tahadhari kwa kupiga honi na king'ora.
Jukwaa la mashabiki wa Mbeya City
lilibaki wazi huku hamasa za kushangilia zikipungua ilhali ndani ya
uwanja wachezaji wa Mbeya City walionekana kupanic kwa kucheza mpira wa
piga nikupige huku wenzao wa Mtibwa wakituliza mpira chini.
Katika hatua nyingine wachezaji wa
Mbeya City walisusia kupanda gari lao na kutembea kwa miguu kutoka nje
ya uwanja kuelekea kambini katika hoteli ya Holiday iliyopo jirani na
uwanja huo.
Mashabiki wa timu hiyo walisikika wakimlaani wazi wazi kocha
wao Juma Mwambusi na kusema kuwa hawamtaki kwa kuwa ameshindwa
kuifundisha timu hiyo.
No comments:
Post a Comment
paulmkale