Chege na Temba waingia studio Afrika Kusini kurekodi wimbo na Uhuru

Wasanii wa TMK, Chege na Temba wako nchini Afrika Kusini ambako wameenda kufanya show kwenye miji ya Pretoria na Johannesburg wakiwa na wasanii wenzao Madee pamoja na Julio.Meneja wa wasanii hao Said Fella wamethibitisha kuwa wakiwa huko Temba na Chege wamefanikiwa kuingia studio na kurekodi ngoma na Uhuru waliotengeneza hits nyingi ikiwemo ‘Khona’ ya Mafikizolo, pamoja na Ole Themba ya Linah kwa hapa Bongo.

“Kikubwa ni kwamba Temba na Chege walifanya show kwanza Pretoria, wakaja kufanya show Johannesburg baadae tukapanga mipango wafanye ngoma na Uhuru, kwahiyo walifanya jana ila leo wanamalizia”.

Fella amesema wimbo huo hawajamshirikisha mtu yeyote, na kuhusu kufanya video huko amesema, “ndo tunafikiria kwasababu Adam yuko kule tulikuwa tunafikiria tufanye na Adam au tufanye na nani”.

No comments:

Post a Comment

paulmkale