Jibu la Diamond la kwanini ametumia tena wazungu kwenye video mpya ‘Ntampata wapi’
Baada ya Diamond kuachia video ya ‘Ntampata wapi’ iliyofanyika Afrika
Kusini, amekutana tena na maswali aliyokutana nayo kipindi alipoachia
video ya..Bofya kuendelea ‘Mdogo mdogo’, ya kwanini amewatumia zaidi wazungu kwenye video
ya wimbo wake wenye ladha ya Kiafrika. Hili ndio jibu la Platnumz baada ya kuulizwa swali hilo kwenye kipindi cha Power Jamz kupitia East Africa Radio:
“Kuna kitu kimoja, waache ubaguzi inategemea na script ya nyimbo
inavyozungumza, script inataka kitu gani, script yangu ya mdogo mdogo
ilikuwa inazungumza kwamba mapenzi hayachagui, ndio maana kulikuwa na
familia ya kizungu mimi familia ya kiafrika, mimi namtaka demu wa
kizungu lakini wazazi wake hawataki, kwahiyo ndo maana mwisho tukaandika
mapenzi hayachagui”.
“Na naamini hicho kitu ndo kilisababisha kufanya hata Marekani
ikashinda tuzo, video ya Aye haikushinda ikashinda video ya Mdogo mdogo
kama video ya Afrika kwasbaabu concept yenyewe ilikuwa inazungumza
vizuri, wazungu wenyewe wameona kama aah hii kweli lakini tuache maswala
ya kibaguzi”.
No comments:
Post a Comment
paulmkale