Kaa Tayari;GOSBY (@thisisgosby) kutambulisha “WEMA SEPETU” leo hii
King
Of Swaghili Rapper Gosby leo ame tease mashabiki wake na cover ya
single yake mpya kama alivyoahidi, Single hiyo inatarajiwa kutoka...> leo
hii.
Rapper
Gosby aka King of Swaghili kutoka Swaghili Nation leo hii anatarajia
kuachia ngoma yake mpya “WEMA SEPETU”. Ngoma hiyo imerekodiwa ndani ya
studio za Feel Good Music na imetengenezwa kwa ushirikiano wa producers
wawili, Jeffrey kutoka Marekani kwa upande wa midundo na Cjamoker kutoka
Tanzania kwa upande wa recording, Mixing and Mastering.
Akiongea
na wanahabari Gosby amesema ameamua kushirikisha producers wa nje na wa
ndani ya nchi ili kuongeza radha kwenye muziki wake na vilevile kupata
uzoefu wa kufanya kazi na watayarishaji tofauti.
“
Muziki wetu unakuwa kwa kasi kubwa, na kama mnavyojua kuwepo kwa
mitandao mbalimbali ya kusambaza kazi zetu online inarahisisha sana kazi
zetu kufika popote dunia, nadhani ni wakati muafaka sasa tukianza
kuangalia soko hili kwa upana zaidi, kuwa na ladha ya bongo na vilevile
kuweka ladha ya kimataifa pia”
Akiongelea
kuhusu wimbohuo unaotarajiwa kutoka mapema leo hii na unaokwenda kwa
jina la “Wema Sepetu “ Gosby alikuwa na haya ya kusema
“
Wema Sepetu, dah sijui nianzie wapi ili iwe rahisi kueleweka, anyways..
Wote tunamjua Wema au tumewahi kusikia au kusoma habari kuhusu Wema, Ni
former Miss Tanzania, Movies Star, Celebrity wa kike ambao anapendwa
sana na watu ndani na nje ya Tanzania. Wanawake wengi wanatamani kuwa
Wema Sepetu kwa ujumla au sehemu tu, na huu wimbo umeongelea juu ya
msichana au mtoto wa kike ambae anafanana na Wema Sepetu.”
Gosby anaendelea
“ Sasa wimbo huu ni special kwa wasichana wote ambao wanafanana na WEMA SEPETU ngoja nisimalize utamu, tega sikio mchana huu.
Kaa tayari kwa kazi hii mpya kutoka kwa Gosby
No comments:
Post a Comment
paulmkale