Kocha Wa Mbeya City Ajihuzulu
Ripoti kadhaa ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa kocha wa timu ya Mbeya City Juma Mwambusi amejiuzulu .
Hatua hiyo imekuja baada ya kuishuhudia timu yake ikipata mfululizo
wa....> matokeo mabaya kwenye ligi ambapo katika michezo saba imeweza
kushinda mchezo mmoja pekee huku ikitoka sare kwenye michezo miwili na
kufungwa jumla ya michezo minne .
Taarifa mbalimbali toka jijini Mbeya zinasema kuwa kwa muda mrefu
wachezaji wa Mbeya City walikuwa wamepoteza Imani na kocha wao hali
ambayo mashabiki wanaamini kuwa imechangiwa na pengo la aliyekuwa kocha
msaidizi wa timu hiyo Maka Mwalusi .
Mwalusi ambaye alihama Mbeya City na kwenda kuifundisha timu ya ligi
daraja la kwanza ya Panoni Fc ya mjini Moshi anadaiwa kutoridhishwa na
kitendo cha kupewa ‘mgao kiduchu’ wa zawadi ya kocha bora ambaye bosi
wake Mwambusi aliipata hali ambayo ilionyesha kutothaminiwa kwa mchango
wake .
Hali ya Juma Mwambusi ilikuwa inaonekana kuwa mbaya kadri Mbeya City
ilivyozidi kupata matokeo mabaya hasa baada ya kujikuta ikipoteza
michezo minne mfululizo mbele ya timu za Azam Fc , Mtibwa Sugar , Mgambo
Jkt na Stand United.
Endapo taarifa hii itathibitika kuwa Kweli Mwambusi ambaye msimu
uliopita alitwaa tuzo ya kocha bora wa msimu kabla ya kutwaa tuzo
nyingine ya kocha bora wa mwezi septemba wakati ligi ilipoanza atakuwa
kocha wa pili kupoteza kibarua chake baada ya Denis Kitambi ambaye
alifukuzwa kazi na Ndanda Fc baada ya matokeo mabaya .
No comments:
Post a Comment
paulmkale