Kampuni
ya Weusi yenye members 5, Joe Makini, Gnako, Nikki wa pili, Bonta na
Lord Eyes, imeazimia kujenga maktaba 100 katika vijiji 100 kwa
kushirikiana na watanzania wengine.Kampeni
itakayofanikisha kujengwa kwa makataba hizo 100 katika vijiji 100
ambazo zitakuwa na vitabu 100 itakuwa inaitwa "MIA Mia Mwanangu" kampeni
ambayo itamuhamasisha mwananchi wa kawaida mwenye kipato cha chini
kushiriki katika kuleta mabadiliko kwa yeye pia kuchangia shilingi 100,
kwahiyo ni kampeni ambayo itachangisha shilingi 100 tu kutoka kwa
mtanzania kwa ajili ya kufikia azimio hilo
unajua
kwasababu sisi tunafunga mwaka na tunakutana na mafans wetu wote
wanaotuunga mkono sehem zote, kwahiyo na sisi tumekaa tukafikiria
tufanye kwaajili ya ku-give back to the community. Toka zamani mi
nilisemaga mi nna idea yangu ya kijiji cha taaluma, ambacho nilisema ni
kutambua machimbo ambayo yapo uswahilini ambayo wanafunzi wanasoma na
kuya-facilitate, lakini sasahivi nikaona hii idea nii-extend nikatafuta
msemo ambao uko uswahilini wa vijana wa kawaida wa watu wa chini
kabisa......." amesema Nikki wa pili
"Nimebuni
hiyo kampeni inayoitwa MIA MIA MWANANGU, ni kampeni rahisi sana
tutajaribu kuhamasisha kila mtu mwenye uwezo wa kuchangia shilingi 100
ambayo nafikiri ni hela ndogo sana lengo nataka tutengeneze makataba
ndogo 100 katika vijiji 100 na kila maktaba itakuwa na vitabu 100...hapa
sasa hivi tunafanya maongezi na jamaa wa sola, tukifanikiwa kwasababu
na wao watakuwa wanatangaza bidhaa zao wanaweka sola pale kwa ajili ya
vijiji ambavyo viko ndani kabisa" ameendelea kusema Nikki ambae ni
msemaji mkuu wa Weusi.
Kwanini shilingi mia na si zaidi na nini umuhimu wa kushiriki katika kampeni hii?
Ni
shilingi mia kwasababu tunataka hata watu wa chini wa-take action
katika kusapoti elimu na kuleta changes, kwasababu tumezoe kuona NGO
mpaka msaada utoke ulaya au watu wa ulaya au sio au watoe msaada watu wakubwa wenye uwezo lakini hata sisi watu wa kipato cha chini tunaweza kuleta mabadiliko katika jamii.......
No comments:
Post a Comment
paulmkale