Diamond na Ommy Dimpoz watajwa kuwania tuzo za HiPipo Music Awards 2015 za Ugand


Mastaa wa Tanzania Nasibu Abdul a.k.a Diamond Platnumz na Omary Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz, nyimbo zao zimetajwa kuwania tuzo za HiPipo Music Awards (HMA2015) za Uganda zinazotarajiwa kutolewa mwakani.Number One’ (original) ya Diamond na ‘Ndagushima’ ya Dimpoz zinachuana na nyimbo zingine za Afrika Mashariki kwenye kipengele kimoja cha East Africa Super Hit.

Nyimbo za Ommy na Diamond zitakuwa zikichuana na ‘Nishike’ ya Sauti Sol na ‘Kioo’ ya Jaguar. Nyimbo nyinginne kwenye kipengele hicho ni Baramushaka – Knowless, Sitya Loss – Eddy Kenzo, Tayali – Urban Boys Ft Iyanya pamoja na Love You Everyday – Bebe Cool.

Tuzo za HiPipo Music Awards 2015 (HMA2015) zitatolewa siku ya Jumamosi Feb.7, 2015

No comments:

Post a Comment

paulmkale