Kauli ya Diamond baada ya kuwanyanyasa wasanii Mombasa
Nimesikitishwa Sana na habari zilizoandikwa na moja ya chombo cha
habari, kuwa eti nliwanyanyasa wasanii wenzangu Nyota ndogo na Susumila,
kwa ...>kuwafukuza kwenye VIP lounge na sijui eti niliwazuia wasitumie maji
ya chupa hivi inaingia akilini kweli hii!!!?? Ningependa kutumia nafasi
hii kuwajulisha mashabiki zangu waliokutana na story hizo kuwa sio za
kweli ni zenye lengo la kudhoofisha Mahusiano yetu mazuri ya wasanii Wa
Africa mashariki..kama BigEye ya Uganda ilivyowahi kuandika habari za
upotoshaji Kati yangu na Jose Chameleone..
Pia
Nawasihi ni vyema mtambue Nafasi yenu kwenye jamii kwa sasa,
Kuweni makini na baadhi ya habari mnazo post ama kureport kutoka baadhi
ya mitandao, zinavunja mahusiano mazuri ya wasanii wa East
Africa...kumbukeni kuna watu wana tabia ya kujudge kitu kwa kusoma
kichwa cha habari tu pasipo kufuatilia undani wa habari...Yawezakuwa
mwaandika kwa nia njema tu, lakini ni vyema muwe mnapata na uhakika
kwanza kabla ya kuripoti, hususan story za kutengeneza chuki kama
hizi....kufanya hivyo ndiyo mtasaidia kukuza industry yetu ya East
Africa...
No comments:
Post a Comment
paulmkale