Arsenal kwenye headlines za kumvuta huyu mkali mwingine!
Klabu ya jijini London ya Arsenal itatangaza kumsajili kiungo wa Real
Madrid Sami Khedira baada ya kufikia makubaliano na wawakilishi wa
mchezaji huyo pamoja na viongozi wa Real Madrid .
Khedira kwa muda mrefu amekuwa hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza
cha Real Madrid hasa baada ya kusajiliwa kwa kiungo Toni Kroos na klabu
ya Arsenal imekuwa ikisaka saini ya kiungo huyu ili kuboresha idara yake
ya kiungo.
Kwa mujibu wa taarifa toka Hispania na England Arsenal imekubali
kulipa paundi milioni 11 kwa ajili ya kiungu huyu mwenye asili ya
Tunisia ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha cha Ujerumani kilichotwaa
ubingwa wa dunia nchini Brazil mwaka jana .Khedira angeweza kuondoka tangu wakati wa usajili wa majira ya joto
lakini Arsenal na Madrid zilishindwa kufikia makubaliano juu yake na
moja kati ya nafasi ambazo zimekuwa zikmtatiza kocha Mfaransa ni nafasi
ya kiungo ambayo Khedira endapo akiwa fiti atakuwa na uwezo wa
kuiboresha .
No comments:
Post a Comment
paulmkale