Manchester City kwenye headlines… wanahusishwa na usajili wa mkali huyu!
Siku chache baada ya kuhusishwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji
raia wa Ivory Coast Wilfred Bony, mabingwa watetezi wa ligi kuu ya
England Manchester City wametajwa kuongoza mbio za kumsajili kiungo wa
Everton Ross Barkley na klabu hiyo imeandaa ofa ambayo ina uhakika kuwa
haitakumbana na kikwazo chochote toka Everton na kwa mchezaji mwenyewe.
Manchester City wanadaiwa kuwa wameandaaa ofa ya paundi milioni 45
kwa ajili ya mchezaji huyo huku wakiwa tayari kumvutia kwa dau nono la
mshahara wa paundi 130,000 kwa wiki kiasi ambacho kitakuwa kinauzidi
mara mbili mshahara wake wa sasa.
Klabu ya Everton kwa upande wake iko tayari kumruhusu Barkley
kuondoka ili mradi ihakikishiwe ada ya uhamisho ya paundi milioni 45
ambazo kwa upande wake itazitumia kuboresha kikosi cha kocha Roberto
Martinez.
Hata hivyo Manchester City watakumbana na vita kali katika mbio za
kumsajili Barkley kwani klabu kadhaa ikiwemo Liverpool zimekuwa
zikimtolea machoHata hivyo itakuwa vigumu kwa Barkley kujiunga na Liverpool
kutokana na
historia ya upinzani wa jadi uliopo baina ya Liverpool na Everton
upinzani ambao mara nyingi hufanya iwe vigumu kwa timu hizo mbili
kubadilishana wachezaji..
No comments:
Post a Comment
paulmkale